Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

ACT Wazalendo Yalaani Shambulio Dhidi ya Padri Dkt. Charles Kitima

  • 39
Scroll Down To Discover

Padre Dr. Charles Kitima, Katibu Mkuu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini (TEC).

Chama cha ACT Wazalendo kimelaani vikali shambulio alilofanyiwa Padre Dkt. Charles Kitima, Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), na kuzitaka mamlaka husika kuchukua hatua za haraka na madhubuti kukomesha matukio ya aina hiyo ambayo hayawezi kuvumiliwa katika jamii.

Kupitia taarifa waliyoitoa kwenye mitandao yao ya kijamii, ACT Wazalendo wamesema kuwa watatoa tamko rasmi kuhusu tukio hilo ndani ya muda mfupi ujao.

Wakati huo huo, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limethibitisha kumshikilia mtu mmoja anayedaiwa kuhusika na tukio hilo. Kwa mujibu wa Kamanda Jumanne Muliro, Padre Kitima alivamiwa na kujeruhiwa kichwani kwa kutumia kitu butu na watu wawili katika eneo la maliwato ya kantini ya TEC, Kurasini, usiku wa kuamkia Mei 1, muda mfupi baada ya kumaliza kikao cha viongozi wa dini kilichodumu kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa moja jioni.

Baada ya kikao hicho, Padre Kitima alibaki katika eneo hilo hadi saa nne na robo usiku ambapo alikwenda maliwatoni na ndipo alipojeruhiwa. Alikimbizwa katika Hospitali ya Aga Khan kwa matibabu na taarifa zinasema hali yake inaendelea kuimarika.

Jeshi la Polisi limemshikilia Rauli Mahabi (pia anafahamika kama Haraja), mkazi wa Kurasini, kwa ajili ya mahojiano kuhusiana na tukio hilo, huku uchunguzi ukiendelea ili kubaini chanzo na kuwachukulia hatua kali wale wote waliohusika.



Prev Post Polepole Akutana na Waziri Mkuu Mlimwa Jijini Dodoma
Next Post Live: Rais Samia Akishiriki Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook