
•Awataka watanzania Wasimame na Dr samia Suluhu
DAR ES SALAAM: Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla amewataka watanzania kuwakataa viongozi wavunja amani.
Pia Makalla amesema inapaswa kuheshimu mihimili yote mitatu ambayo ni Serikali, Bunge na Mahakama na kuachana na watu wanaofanya uvunjifu wa sheria kwani hakuna ambaye aliyejuu ya sheria.
Makalla ambaye pia ni mlezi wa CCM katika Mkoa wa Dar es salaam ameeleza ayo leo Aprili 29,2025 wakati akizungumza na wananchi katika uwanja wa Mwananyama kwa Kopa Wilaya ya Kinondoni Dar es salaam.ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya siku tatu katika mkoa huo.
Makalla amesema uvunjaji wa sheria Tanzania sio mahali pake na badala yake watu wanapaswa kuheshimu mihimili yote mitatu tajwa kwani hakuna mtanzania yoyote yule aliye juu ya sheria.
“Chokochoko, uvunjai wa sheria si mahali pake tunapaswa kuheshimu mihimili yote ya serikali, mahakama Bunge na serikali hakuna mtanzania aliye juu ya sheria, kwahiyo niwaombe watanzania tuendelee kulinda amani,” amesema Makalla.
Makalla amesisitiza katika kuheshimu mihimili hiyo mahakama iachwe ili iweze kufanya maamuzi kwa uhuru na haki kwani mahakam ni chombo huru.
Aidha Makalla amesema kuwa chama kimoja hakiwezi kuvunja katiba na sheria wala kuwanyima watanzania wengine haki yao ya kushiriki uchaguzi kama katiba inavyoelekeza.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!