MAGAZETI ya Leo Jumatano 30 April 2025
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF), Jenerali Jacob Mkunda Aprili 29, 2025 amehitimisha mafunzo ya Askari wapya katika shule ya Mafunzo ya Awali ya Kijeshi iliyopo Kihangaiko, Msata wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.
Askari waliohitimu mafunzo hayo wamekula kiapo cha utii mbele ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF).
Akizungumza wakati wa sherehe hizo, Jenerali Mkunda amewataka Askari wapya kwenda kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia kiapo cha utii na kuwajibika kulinda mipaka ya nchi, kuilinda Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kumtii Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu.
Askari wapya wametakiwa kutunza afya zao kwa kuwa muda wote wanatakiwa kuwa na utimamu wa afya ili waweze kulitumikia Taifa kama walivyokusudiwa.
Aidha, Jenerali Mkunda amewaasa Askari kuzingatia mambo manne kwa Mwanajeshi ambayo ni nidhamu nzuri, utii, uhodari na uaminifu kwani Taifa linawaamini na kuwategemea katika ulinzi.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!