Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Stanbic Yazindua Kampeni ya Kupanda miti 50,000 Tanzania Kuadhimisha Siku ya Dunia

  • 6
Scroll Down To Discover

Omari Mtiga, Mkuu wa Wateja Binafsi na Wateja Maalum wa Benki ya Stanbic, akipanda mti kuadhimisha Siku ya Dunia (International Earth Day) kupitia kampeni ya Blue Roots, inayolenga kupanda miti 50,000 nchini Tanzania.

Benki ya Stanbic Tanzania imezindua kampeni ya upandaji miti itakayohusisha miti 50,000 nchini, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya Dunia na juhudi za kulinda mazingira.

Kampeni hiyo, inayojulikana kama Blue Roots, ni sehemu ya mkakati mpana wa Standard Bank barani Afrika wa kupanda miti milioni moja. Lengo lake ni kuunganisha ukuaji wa uchumi na ulinzi wa mazingira kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo, huku ikihamasisha ushiriki wa sekta binafsi na jamii kwa ujumla.

Uzinduzi wa kampeni hiyo umefanyika katika makao makuu ya benki jijini Dar es Salaam, ambapo viongozi na wafanyakazi wa Stanbic walishiriki zoezi la upandaji miti kama ishara ya dhamira ya taasisi hiyo katika kuendeleza maendeleo yanayozingatia mazingira.

Kwa mujibu wa benki hiyo, katika kipindi cha zaidi ya miaka 30 ya uwepo wake nchini, imeendelea kuchangia ukuaji wa uchumi kwa kusaidia biashara na kurahisisha shughuli za kifedha. Kupitia kampeni ya Blue Roots, Stanbic inalenga kuendeleza mchango huo kwa kuunganisha maendeleo ya kiuchumi na uhifadhi wa mazingira.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa hatua ya kupanda miti milioni moja barani Afrika inalenga kutambua mchango wa sekta binafsi katika kujenga mustakabali endelevu huku ikilinda mifumo ya ikolojia inayochochea ukuaji huo.

Nchini Tanzania, Stanbic tayari imepanda miti 102,850 katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, ikiwa ni sehemu ya jitihada zake za kuboresha mazingira na kuongeza uelewa wa jamii kuhusu umuhimu wa uhifadhi wa mazingira.

Wataalamu wanaeleza kuwa upandaji miti una mchango mkubwa katika kuboresha ubora wa hewa, kulinda rutuba ya udongo na kuhifadhi vyanzo vya maji, pamoja na kuboresha mazingira ya maisha ya jamii.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkuu wa Wateja Binafsi na Wateja Maalum wa benki hiyo, Omari Mtiga, alisema Stanbic imeendelea kukua pamoja na Tanzania huku ikichangia maendeleo ya taifa.

“Tunataka kuhakikisha kuwa ukuaji wa uchumi unaenda sambamba na ulinzi wa mazingira ili kuacha thamani ya kudumu kwa jamii,” alisema.

Kwa upande wake, Meneja Uendelevu wa benki hiyo, Annette Nkini, alisema upandaji miti ni uwekezaji muhimu kwa jamii na kwa vizazi vijavyo.

“Tunataka kuona matokeo yanayoonekana katika maisha ya watu na mazingira kupitia programu zetu,” alisema.

Kampeni ya Blue Roots inatarajiwa kutekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini kwa kushirikisha wafanyakazi wa benki, wateja pamoja na jamii, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kulinda mazingira na kuendeleza maendeleo ya taifa.

The post Stanbic Yazindua Kampeni ya Kupanda miti 50,000 Tanzania Kuadhimisha Siku ya Dunia appeared first on Global Publishers.



Prev Post Rais Samia Akabidhi Mitungi ya Oryx kwa Mama na Baba Lishe Dar es Salaam
Next Post Video ya CCTV Ikimuonesha Bodaboda Aliyeiba Mtoto Mwanza, Apatikana Akiwa Hai
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook