Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Polisi Wamuita Hilda Newton Baada ya Madai Mazito Kumhusu Tundu Lissu

  • 5
Scroll Down To Discover

Jeshi la Polisi limesema linaendelea na uchunguzi baada ya kupokea taarifa zinazohusiana na chapisho la Hilda Newton alilolitoa na kulisambaza katika mitandao ya kijamii tarehe 10 Aprili 2026.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Hilda Newton alidai katika chapisho lake kuwa Serikali imepanga kumuua Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu kwa njia ya risasi, madai ambayo yamechukuliwa na mamlaka za uchunguzi kama suala linalohitaji kufanyiwa uhakiki na ushahidi wa kina.

Jeshi la Polisi limesema linaendelea kukusanya ushahidi kuhusiana na tuhuma hizo ili kubaini ukweli wake, na limemwelekeza Hilda Newton kufika katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) zilizopo Makao Makuu Ndogo ya Polisi, Mtaa wa Ohio jijini Dar es Salaam, tarehe 24 Aprili 2026 saa 4:00 asubuhi.

Kwa mujibu wa polisi, hatua hiyo inalenga kumpa nafasi mhusika kuwasilisha ushahidi anaodai kuhusiana na taarifa aliyoisambaza kwa umma kupitia mitandao ya kijamii.

Jeshi la Polisi limesema hatua hiyo inafanyika kwa mujibu wa kifungu cha 11 (2) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, kama kilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2023.

Uchunguzi huo unaendelea huku mamlaka zikisisitiza umuhimu wa kufuata taratibu za kisheria katika kushughulikia taarifa za aina hiyo zinazohusisha masuala ya usalama wa watu na taasisi.

The post Polisi Wamuita Hilda Newton Baada ya Madai Mazito Kumhusu Tundu Lissu appeared first on Global Publishers.



Prev Post Je, Iran itashiriki mazungumzo ya amani na Marekani? Katika Dira ya Dunia TV
Next Post Trump Aongeza Muda wa Mapigano Kusitishwa, Pakistan Yatoa Shukrani
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook