MWANARIADHA nyota wa Tanzania, Alphonce Simbu, amewashukuru Watanzania kwa sapoti kubwa waliompa iliyomuwezesha kufanya vizuri katika mbio za Boston Marathon 2026, ambako alimaliza katika nafasi ya pili na kuweka rekodi mpya ya kitaifa.
Akizungumza mara baada ya kumaliza mbio hizo , Simbu amesema mafanikio hayo yametokana kwa kiasi kikubwa na maombi na hamasa kutoka kwa Watanzania waliokuwa wakimuunga mkono.
“Kwa Watanzania wenzangu, kutoka moyoni mwangu, asanteni sana. Kusimama kwenye jukwaa la washindi ni heshima ninayoshiriki nanyi nyote. Maombi yenu na sapoti yenu yamenibeba katika kila hatua ya mbio,” amesema Simbu.
Ameongeza kuwa kutwaa medali ya fedha sambamba na kuweka rekodi mpya ya taifa ya saa 2:02:47 si mafanikio yake binafsi pekee, bali ni ushindi wa Watanzania wote.
“Kurejea nyumbani na medali ya fedha pamoja na rekodi mpya ya taifa ya saa 2:02:47 ni ushindi wa nchi yetu sote,” amesema
Simbu amebainisha kuwa mafanikio hayo yameonesha uwezo na ushindani wa Watanzania katika jukwaa la kimataifa, akieleza kuwa hiyo ni hatua ya mwanzo kuelekea mafanikio makubwa zaidi yajayo.
“Tumeonesha dunia nguvu ya Mtanzania, huu ni mwanzo tu,” amesema Mwanariadha huyo.
The post MTANZANIA ATIKISA DUNIA KWA REKODI MPYA BOSTON appeared first on Soka La Bongo.











Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!