Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Rais aonya wafanyabiashara kupandisha bei kiholela kisa kupanda kwa mafuta

  • 4
Scroll Down To Discover

Rais Samia Suluhu Hassan, amewataka wafanyabiashara nchini kuwa waadilifu katika kipindi hiki cha kupanda kwa bei ya mafuta duniani na kupanga bei za badhaa kwa kuzingatia uhalisia wa gharama.

Ameyasema hayo Ikulu Chamwino jijini Dodoma wakati wa hafla ya kuwaapisha viongozi mbalimbali, ambapo amesema baadhi ya bidhaa zilizopo maghalani zilinunuliwa kabla ya kupanda kwa bei ya mafuta, hivyo wafanyabiashara wanapaswa kuangalia namna ya kurekebisha bei bila kuwaumiza wananchi.

“Isitumike fursa ya kupanda kwa mafuta na kuweka bei za bidhaa kubwa kuliko zinavyopaswa kuwa. Lakini wananchi pia, kuna bidhaa ambazo zinaingia kipindi hiki ambazo zimekumbana na msukosuko huu zitapanda bei,” amesema.

Aidha, Rais Samia amebainisha kuwa hali hiyo siyo tatizo la Tanzania pekee bali ni changamoto ya dunia nzima, huku akiwaomba wananchi kuwa watulivu na kuendelea kuomba juu ya maendeleo ya hali ya kimataifa, ikiwemo mvutano unaoathiri usafirishaji wa mafuta duniani.

The post Rais aonya wafanyabiashara kupandisha bei kiholela kisa kupanda kwa mafuta appeared first on SwahiliTimes.



Prev Post TBL YATOA WITO WA HATUA ZA PAMOJA ZA KUKABILIANA NA HATARI ZA POMBE HARAMU TANZANIA
Next Post Benki ya Exim Yaingia Ubia wa Kimkakati na The Voice TZ Kwa Lengo la Kukuza Matumizi ya Malipo ya Kidijitali Nchini Tanzania
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook