Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Serikali kuwarasimisha na kuwawezesha mama na baba lishe

  • 2
Scroll Down To Discover

Rais Samia Suluhu Hassan amesema serikali itaendelea kuchukua hatua za kuweka mikakati mahususi ya urasimishaji na uwezeshaji wa biashara ndogondogo, ikiwemo kundi la Mama na Baba Lishe, ili waweze kuwa sehemu muhimu ya utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Akizungumza leo na wadau wa sekta hiyo amesema biashara ndogondogo zina mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa nchi na kutoa ajira kwa wananchi wengi, hivyo serikali imejipanga kuhakikisha zinapata mazingira bora ya kufanya kazi na kuendelea kukua.

“Serikali itaendelea kuchukua hatua za kuweka mikakati mahususi ya urasimishaji na uwezeshaji wa biashara ndogondogo ikiwemo kundi la Mama na Baba Lishe ili muweze kuwa sehemu muhimu ya utekelezaji wa Dira ya 2050,” amesema Rais Samia.

Aidha, amesema serikali itaendelea kuimarisha mifumo ya uwezeshaji wananchi kiuchumi kupitia utoaji wa mikopo mbalimbali ili kuwezesha upatikanaji wa mitaji pamoja na huduma zote muhimu kwa wafanyabiashara wadogo.

Ameeleza kuwa dhamira ya serikali ni kuona wananchi wengi zaidi wanashiriki kikamilifu katika shughuli za uzalishaji mali na kunufaika na fursa za kiuchumi zinazojitokeza nchini.

The post Serikali kuwarasimisha na kuwawezesha mama na baba lishe appeared first on SwahiliTimes.



Prev Post ‎MAKONDA: ACHENI KUBEZA NCHI, JENGENI TASWIRA CHANYA KUVUTIA FURSA
Next Post BENKI YA EQUITY TANZANIA YAZINDUA TAWI JIPYA LA UBUNGO LILILOPO EACLC JIJINI DAR ES SALAAM
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook