Rais Donald Trump anadai kwamba “Rais wa Serikali Mpya ya Iran” ameomba Marekani kusitisha mapigano. Lakini Iran imepuuzilia mbali madai hayo ikisema kwamba ni ya uwongo na yasiyo na msingi. Trump Hakumtaja kiongozi huyo mkuu wa Iran kwa jina, lakini alimuelezea kuwa mtu “asiye na msimamo mkali na mwenye busara zaidi kuliko viongozi waliomtangulia.” Aliongeza kuwa: “Tutazingatia ombi hilo wakati mlango wa bahari wa Hormuz utakapokuwa wazi na huru. Hadi wakati huo, tunaendelea kuishambulia Iran hadi iangamie kabisa!!” mwisho wa nukuu.
#iran #DonaldTrump #BBCSwahili #BBCSwahiliLeo
Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw









Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!