

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mahmoud Thabit Kombo amempokea Makama wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango jijini Roma, Italia ambapo atamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Misa ya Mazishi ya aliyekuwa Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani Baba Mtakatifu Francisko itakayofanyika katika Mji wa Vatican Aprili 26, 2025.
Katika mapokezi hayo Waziri Kombo aliambatana na Balozi wa Tanzania katika Mji wa Vatican mwenye makazi yake nchini Ujerumani, Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika (DEA) katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushikiano wa Afrika Mashariki Balozi Swahiba Mndeme, na watendaji wengeni wa Serikali.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!