Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Baharia wa Marekani Ahukumiwa kwa Ujasusi kwa Niaba ya China

  • 2
Scroll Down To Discover

Baharia wa Jeshi la Wanamaji la Marekani, Jinchao Wei (25), amehukumiwa nchini California kwa kosa la ujasusi baada ya kupatikana na hatia ya kuuza siri za kijeshi kwa afisa wa China aliyemsajili kupitia mitandao ya kijamii.

Wei, anayejulikana pia kama Patrick Wei, alipatikana na hatia ya makosa sita ikiwemo ujasusi, njama ya kufanya ujasusi na usafirishaji haramu wa taarifa za siri. Alikamatwa Agosti 2023 akiwa njiani kuanza kazi kwenye meli ya mashambulizi ya amphibious, USS Essex.

Mwanasheria wa Marekani, Adam Gordon, alisema kuwa kitendo cha Wei kilikuwa “usaliti mkubwa wa uaminifu aliopewa kama mwanajeshi wa Marekani” na kwamba aliweka hatarini usalama wa taifa na washirika wake kwa kubadilisha siri za kijeshi kwa fedha taslimu.

Kwa mujibu wa ushahidi uliowasilishwa mahakamani, Wei alikuwa akitumiana jumbe, simu na mawasiliano ya kisiri na afisa wa China aliyemtambulisha kama “Big Brother Andy”. Alijaribu kuficha mawasiliano hayo kwa kutumia programu zilizowekwa usimbaji wa hali ya juu, simu na kompyuta mpya alizopewa na mhudumu wake huyo.

Kama fundi mitambo mwenye kibali cha usalama, Wei alipata taarifa nyeti kuhusu meli za kivita katika eneo la Pasifiki, na kwa muda mrefu alishirikiana na afisa huyo wa Kichina kwa malipo ya kifedha.

Hukumu yake imekuwa ishara ya tahadhari kubwa kuhusu jitihada za ujasusi wa China dhidi ya Marekani, hususan ndani ya vikosi vya kijeshi.



Prev Post PITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO AGOSTI 21, 2025
Next Post Afrika Yaongoza Dunia kwa Vifo vya Ajali za Barabarani, Sababu Kuu Zafichuliwa
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook