
Ibada ya mazishi ya Papa Francis inafanyika leo Jumamosi katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican, ambapo mamia kwa maelfu ya waombolezaji wanatarajiwa kuhudhuria, wakiwemo viongozi wa dunia, familia za kifalme na maafisa wa Kanisa Katoliki.
Shughuli ziitaanza saa 10:00 kwa saa za huko sawa na saa 7 mchana kwa saa za Afrika Mashariki na inatarajiwa kudumu kwa karibu saa moja na nusu. Baada ya misa kumalizika, mwili wa Francis utasafirishwa hadi katika kanisa la Santa Maria Maggiore mjini Roma kwa mazishi. Baada ya hap Kipindi cha maombolezo cha siku tisa kitaanza.
Wakuu wengi wa nchi na familia ya kifalme wamethibitisha kuhudhuria mazishi hayo, wakiwemo Mwanamfalme William wa Uingereza, Rais wa Marekani Donald Trump, Mfalme wa Uhispania Felipe VI na Malkia Letizia na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!