Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Waziri Mkuu Akagua Ukarabati Wa Uwanja Wa Ndege Wa Sumbawanga

  • 33
Scroll Down To Discover

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba Machi 08, 2026 amekagua maendeleo ya ukarabati na uboreshaji wa Uwanja wa Ndege wa Sumbawanga uliopo mkoani Rukwa.

Mradi huo ulianza kutekelezwa katika mwaka wa fedha 2023/2024 kwa gharama ya shilingi bilioni 60.1 na hadi sasa umefikia asilimia 96 ya utekelezaji.

Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, Dkt. Mwigulu amewapongeza wananchi wa Rukwa kwa kupata uwanja wa ndege wa kisasa kwa kuwa maendeleo hayo yanaonesha mabadiliko makubwa ya mkoa huo.

Amesema kuwa kwasasa Rukwa siyo ile ya zamani bali ni Rukwa ya kisasa na ya viwango, inayokwenda sambamba na kasi ya maendeleo ya taifa.

Aidha, amesema miradi ya aina hiyo ndiyo mafanikio ambayo Serikali ya Awamu ya Sita inajivunia kwa kuwekeza katika miradi ya maendeleo yenye tija na inayoacha alama kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

Ukarabati na upanuzi wa uwanja huo unatarajiwa kuimarisha huduma za usafiri wa anga katika Ukanda wa Nyanda za Juu Kusini pamoja na kuchochea shughuli za kiuchumi na kijamii.

Mheshimiwa Dkt. Mwigulu ameanza ziara ya kikazi katika mkoa wa Rukwa ambapo atakagua miradi ya maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi.

The post Waziri Mkuu Akagua Ukarabati Wa Uwanja Wa Ndege Wa Sumbawanga appeared first on Global Publishers.



Prev Post Mojtaba Khamenei Achaguliwa Kuwa Kiongozi Mkuu Mpya wa Iran
Next Post PITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO MACHI 09, 2026
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook