Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

SOWAH KITANZINI, SAA 72 KUJITETEA SIMBA

  • 25
Scroll Down To Discover

UONGOZI wa Simba SC umemtaka mshambuliaji wake, Jonathan Sowah, kutoa majibu rasmi ndani ya saa 72 sawa na siku tatu kuhusiana na tuhuma mbalimbali za kinidhamu zinazomkabili ndani ya klabu hiyo.

Imeelezwa kuwa nyota huyo amefikishwa mbele ya Kamati ya Nidhamu ya klabu, huku akitakiwa kuwasilisha majibu yake ndani ya muda uliotolewa. Wakati huo huo, adhabu yake ya kusimamishwa na kutokuwa sehemu ya kikosi cha timu inaendelea hadi uchunguzi wa kina utakapokamilika.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya klabu, uongozi wa Simba unahitaji maelezo ya kina kutoka kwa mchezaji huyo kuhusu vitendo kadhaa vinavyodaiwa kukiuka taratibu na nidhamu ya timu. Hatua hiyo inaelezwa kuchukuliwa kwa lengo la kulinda misingi ya uwajibikaji, heshima na nidhamu ndani ya kikosi hicho.

Chanzo kutoka ndani ya klabu kimeeleza kuwa miongoni mwa mambo anayopaswa kuyafafanua Sowah ni madai ya kufika kuchelewa kwenye mikutano ya timu pamoja na vipindi vya mazoezi, hali inayodaiwa kujirudia mara kadhaa na kuzua maswali kutoka kwa benchi la ufundi na uongozi wa klabu.

Mbali na hilo, mshambuliaji huyo pia anatuhumiwa kukataa kushiriki mazoezi ya ziada maarufu kama top-up sessions ambayo huandaliwa na benchi la ufundi kwa lengo la kuboresha utimamu wa mwili na kiwango cha wachezaji.

Sowah pia anatakiwa kutoa maelezo kuhusu tukio la kusafiri kwenda Angola akiwa amevaa jezi ya SL Benfica badala ya mavazi rasmi ya klabu, jambo linalodaiwa kwenda kinyume na taratibu za utambulisho wa timu wakati wa safari za kikazi.

Aidha, klabu hiyo inahitaji ufafanuzi wake kuhusu madai ya kufanya makosa ya makusudi uwanjani yanayoweza kusababisha adhabu kali kama kadi nyekundu. Matukio hayo yanatajwa kujitokeza katika baadhi ya michezo, ikiwemo dhidi ya Azam FC pamoja na Espérance Sportive de Tunis.

Inaelezwa kuwa baada ya kupokea majibu ya mchezaji huyo ndani ya muda uliowekwa, uongozi wa Simba utafanya tathmini na kuchukua hatua stahiki kulingana na kanuni na taratibu za klabu.

Hivi karibuni, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Crescentius Magori, amesema  kuwa endapo mchezaji huyo atabainika kuwa na makosa, klabu haitasita kuchukua hatua kali za kinidhamu ikiwemo adhabu au kukatwa sehemu ya mshahara wake.

The post SOWAH KITANZINI, SAA 72 KUJITETEA SIMBA appeared first on Soka La Bongo.



Prev Post DAR ES SALAAM DERBY HAITAWEZEKANA BILA FEITOTO
Next Post SIMBA WAFUNGUA VITA KOMBE CRDB, B19 KWENYE MTEGO
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook