KIUNGO wa Azam FC, Feisal Salum maarufu kama Fei Toto, anatarajiwa kurejea kikosini na kuanza kucheza katika michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwemo ule dhidi ya Dodoma Jiji FC pamoja na dabi ya jijini dhidi katianga.
Fei Toto anakosa michezo miwili ya Azam FC, ukiwemo wa leo dhidi ya Tanzania Prisons FC katika ligi pamoja na mchezo wa hatua ya 32 bora ya CRDB Federation Cup dhidi ya Mbeya Kwanza FC, kutokana na kutumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyopata katika mchezo dhidi ya Pamba Jiji FC.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Azam FC, Heshim Ibwe, kiungo huyo atakosekana katika michezo hiyo miwili pekee kabla ya kurejea uwanjani baada ya kumaliza adhabu yake.
“Fei Toto anakosa mechi mbili, ya leo dhidi ya Tanzania Prisons na ule wa Mbeya Kwanza katika Kombe la Shirikisho la CRDB. Baada ya hapo atakuwa amemaliza adhabu yake na ataweza kucheza michezo inayofuata ikiwemo dhidi ya Dodoma Jiji na Yanga,” amesema Ibwe.
Ibwe ameongeza kuwa kiungo huyo anaendelea vizuri na mazoezi ya timu ili kujiweka katika kiwango bora cha utimamu wa mwili, akilenga kurejea kwa nguvu kwenye kikosi cha Azam FC katika michezo muhimu ijayo.
Kurejea kwa Fei Toto kunatarajiwa kuipa nguvu zaidi Azam FC hasa kuelekea michezo mikubwa ya ligi, ikiwemo dabi ya Dar es Salaam dhidi ya Yanga ambayo huwa na ushindani mkubwa kila msimu.
The post DAR ES SALAAM DERBY HAITAWEZEKANA BILA FEITOTO appeared first on Soka La Bongo.






Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!