Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

TBS Kanda ya Kaskazini Yahakikisha Ubora wa Bidhaa na Vifaa vya Miradi ya AFCON

  • 14
Scroll Down To Discover

Meneja wa Kanda ya Kaskazini (TBS), Mhandisi Ismail Mwaipaja

Meneja wa Kanda ya Kaskazini (TBS), Mhandisi Ismail Mwaipaja, amezungumza na waandishi wa habari mapema leo Marchi 06, 2026 Jijini Arusha kuhusu mafanikio na utekelezaji wa majukumu ya kanda hiyo.

Mhandisi Mwaipaja amesema TBS Kanda ya Kaskazini imefanikiwa kuthibitisha ubora wa bidhaa za wazalishaji pamoja na wajasiriamali 492, ambapo kati yao 238 ni wajasiriamali wadogo. Hatua hiyo imechangia kwa kiasi kikubwa kukuza uchumi na kuhakikisha soko linakuwa na bidhaa bora na salama kwa watumiaji.

Aidha, ameeleza kuwa TBS inaendelea kuboresha huduma na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma zake, ikiwa ni pamoja na mpango wa kujenga maabara mpya jijini Arusha ili kurahisisha upimaji na uthibitishaji wa ubora wa bidhaa.

Vilevile, TBS imeendelea kutoa mchango katika kuhakikisha ubora wa vifaa vinavyotumika katika miradi mikubwa ya maendeleo nchini, ikiwemo miradi ya ujenzi wa miundombinu ya michezo inayohusiana na maandalizi ya michuano ya Africa Cup of Nations (AFCON), kwa kuhakikisha vifaa vya ujenzi vinakidhi viwango .

Na Neema Adrian – GPL

KATIKATI YA MAKOMBORA ya ISRAEL GAZA ANAZALIWA BINTI MLEMAVU WA MACHO MWENYE KIPAJI CHA KUVUTIA…

The post TBS Kanda ya Kaskazini Yahakikisha Ubora wa Bidhaa na Vifaa vya Miradi ya AFCON appeared first on Global Publishers.



Prev Post Fahamu Hadithi ya Zein Al-Dalou: Msichana Asiyeona Aliyehifadhi Qur’ani Wakati wa Vita Gaza – Video
Next Post Simba Yatozwa Faini ya Milioni 10 Baada ya Dabi ya Kariakoo Zanzibar
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook