Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

SIMBA YAWASHA ALARM, DODOMA JIJI SI SAWA NA PRISONS

  • 54
Scroll Down To Discover

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa unatarajia upinzani mkali kutoka kwa Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaochezwa kesho kwenye Uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, amesema kikosi hicho hakiingii uwanjani kwa dharau, kikitambua wazi kuwa Dodoma Jiji ni wapinzani wenye ushindani mkubwa kuliko Tanzania Prisons, ambao Simba iliwafunga mabao 2-0 katika mechi iliyopita.

Ahmed amesisitiza kuwa Dodoma Jiji ni timu inayocheza kwa nidhamu na ushindani wa hali ya juu, na imekuwa ikiisumbua Simba mara kwa mara wanapokutana, iwe ni nyumbani au ugenini.

“Mechi ya Dodoma Jiji ni ngumu zaidi. Kama kuna aliyeona ushindani tulioupata dhidi ya Prisons ulikuwa mkubwa, basi ajue wa Dodoma Jiji utakuwa mkubwa zaidi. Ukiangalia ubora wa timu hizi mbili, Dodoma wako juu,” amesema Ahmed.

Ameongeza kuwa rekodi za misimu mitatu iliyopita zinaonyesha wazi ugumu wa mpinzani huyo, kwani mara nyingi Simba imekuwa ikipata ushindi mwembamba wanapokutana, hali inayoonesha uimara wa Dodoma Jiji.

“Sisi wenyewe tumekuwa tukiwafunga Dodoma Jiji kwa tabu sana, mara nyingi ushindi wa bao 1-0 kwa misimu kadhaa. Hii si bahati mbaya, ni matokeo ya ubora wao,” amesisitiza.

Ahmed amegusia changamoto ya kucheza ugenini katika Uwanja wa Jamhuri, akieleza kuwa sapoti ya mashabiki wa nyumbani inaweza kuongeza presha kwa wachezaji wa Simba. Hata hivyo, ameweka bayana kuwa malengo yao ni kuondoka na pointi tatu muhimu.

Simba inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na dhamira ya kuendelea kujiweka katika nafasi nzuri kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ikitambua kuwa ushindi dhidi ya Dodoma Jiji utakuwa na uzito mkubwa katika safari yao ya msimu huu.

The post SIMBA YAWASHA ALARM, DODOMA JIJI SI SAWA NA PRISONS appeared first on Soka La Bongo.



Prev Post YANGA WAMTEGEMEA DEPU KUBEBA TIMU, DERBY
Next Post Rais Mstaafu Kikwete Akabidhi Tuzo za Viongozi Bora Barani Afrika 2026
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook