Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

YANGA YAFICHUA MPANGO WA SIRI KABLA YA DABI

  • 20
Scroll Down To Discover

WAKATI mashabiki wa Yanga  wakishangazwa na kiwango kilichoonyeshwa na timu yao katika mchezo uliopita, Ofisa Habari wa klabu hiyo, Ali Kamwe, ameweka mambo hadharani akieleza kuwa walikuwa na mipango maalum iliyolenga ratiba yao ijayo.

Kamwe amesisitiza kuwa Namungo FC si timu ndogo kama baadhi wanavyodhani, akibainisha kuwa Wananchi wapo kwenye kipindi kigumu chenye mechi mfululizo zenye ushindani mkubwa.

Amesema kabla ya kufika kwenye Kariakoo Derby, bado wana kibarua kizito dhidi ya JKT Tanzania, hivyo walilazimika kuangalia picha pana zaidi ya msimu wao.

Kauli hiyo imekuja kufuatia baadhi ya mashabiki kutoridhishwa na namna timu yao ilivyocheza, huku wengi wao tayari wakiwa na mawazo kuelekea mchezo wa Machi Mosi dhidi ya watani zao Simba SC, utakaopigwa katika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

“Unaelekea kwenye Dabi halafu unacheza na Namungo inayofundishwa na Mgunda, ukipata alama tatu sema Alhamdulillah, wakubwa watakuwa wamenielewa.

Bado tuna kibarua dhidi ya JKT. Hizi mechi mbili ni ngumu kuliko Derby yenyewe kwa sababu zina macho ya watu wengi,” amesema Kamwe.

Ameongeza kuwa kiwango kilichoonekana si ajali, bali ni sehemu ya mkakati wao wa kujiandaa vyema na michezo hiyo miwili muhimu.

“Tunawatazama wanaosema tumeshuka kiwango, ni kweli hatukucheza kama tulivyozoeleka, lakini tuna mipango yetu. Kuelekea Kariakoo Derby ni suala la muda, kule Zanzibar kila kitu kitaonekana,” ameongeza.

Kwa sasa kikosi cha Yanga kinatarajiwa kurejea jijini Dar es Salaam kikitokea Ruangwa, mkoani Lindi, kwa ajili ya kujiandaa na mchezo ujao wa Februari 25, 2026 dhidi ya JKT Tanzania, kabla ya kuelekeza nguvu zote kwenye dabi inayosubiriwa kwa hamu kubwa.

The post YANGA YAFICHUA MPANGO WA SIRI KABLA YA DABI appeared first on Soka La Bongo.



Prev Post BARKER AWEKA MKAKATI KABISA, SIMBA WAZINDUA SILAHA
Next Post BARKER AWEKA WAZI SIRI YA HOFU, KABLA YA DERBY
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook