KOCHA Mkuu wa Simba SC, Steve Barker, ameanza maandalizi kwa umakini mkubwa kuelekea mchezo unaosubiriwa kwa hamu, Kariakoo Derby dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga SC, utakaopigwa Machi Mosi visiwani Zanzibar.
Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkali, huku pande zote mbili zikihitaji ushindi si tu kwa heshima, bali pia katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Barker ameamua kuanza kusuka mkakati thabiti wa kuwazidi wapinzani wake, akitumia nyota wake muhimu kama silaha kuu.
Katika maandalizi haya, kocha huyo anategemea silaha tano za msingi zitakazokuwa na mchango mkubwa kuvunja safu ya ulinzi ya Yanga.
Nyota hao ni Inno Loemba, Clatous Chama, Libasse Gueye, Selemani Mwalimu, na Anicet Oura, ambao kila mmoja amekuwa na mchango muhimu katika michezo ya hivi karibuni ya Simba.
Kiungo mshambuliaji Chama amejulikana kama injini ya ubunifu wa Simba, akiwa na uwezo wa kutengeneza nafasi na kufunga mabao nyakati muhimu. Uzoefu wake katika mechi zenye presha kama Derby unampa Barker imani kubwa kuwa anaweza kubadilisha matokeo kwa wakati wowote.
Kwa upande wa Loemba na Oura, kasi na nguvu zao katika kushambulia ni mtaji mkubwa kwa Simba. Wana uwezo wa kupenya pembeni, kuwasumbua mabeki wa Yanga, na kufungua mianya ya mabao mapema, jambo linaloweza kuipa timu hiyo faida ya mapema katika mchezo.
Naye Gueye anachukua jukumu la kumalizia kazi. Uwezo wake wa kusimama imara ndani ya boksi na kutumia vyema nafasi chache atakazopata unaweza kuwa silaha ya mwisho ya Simba katika pambano hilo linalosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka nchini.
Kwa ujumla, Barker anaonekana tayari kimastratejia, akijumuisha ubunifu, kasi, na umaliziaji makini. Mchanganyiko huu unalenga kuipa Simba ushindi muhimu katika Derby ya kihistoria itakayochezwa Zanzibar, mashabiki wakitarajia mchezo wa kuchomeka presha na burudani isiyosahaulika.
The post BARKER AWEKA MKAKATI KABISA, SIMBA WAZINDUA SILAHA appeared first on Soka La Bongo.






Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!