Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Tundu Lissu Apinga Ushahidi Mpya Katika Kesi ya Uhaini

  • 16
Scroll Down To Discover

Malumbano makali ya hoja yameibuka mahakamani katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, kufuatia hatua ya Jamhuri kuwasilisha notisi ya kuongeza ushahidi mpya.

Leo, Jumatatu Februari 23, 2026, upande wa mashtaka umeieleza Mahakama kuwa Februari 18, 2026 uliwasilisha kwa njia ya mtandao notisi ya kuongeza ushahidi katika kesi hiyo.

Wakili wa Serikali Mkuu, Nassoro Katuga, amesema notisi hiyo imewasilishwa kwa mujibu wa kifungu cha 308(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), Marejeo ya mwaka 2023. Amesema Jamhuri haiombi kuongeza shahidi mpya, bali inaomba kuongeza ushahidi mpya katika ushahidi wa shahidi wao, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Amin Mahamba, na kwamba kiini cha ushahidi huo kimeambatanishwa.

Hata hivyo, Lissu amepinga vikali hatua hiyo, akisisitiza kuwa kifungu cha 308 cha CPA kinahusu shahidi mpya na si ushahidi mpya wa shahidi aliyekwisha kutoa ushahidi. Amesema shahidi mpya ni yule ambaye maelezo yake au ushahidi wake haukuwahi kusomwa katika mwenendo wa awali wa kesi.

Aidha, Lissu ametahadharisha kuwa yuko tayari kujadili hadharani yaliyotokea katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, akidai kuwa kuingiza ushahidi unaohusiana na mchakato huo kunaweza kufungua mjadala mpana ambao, kwa mujibu wake, dunia inapaswa kuujua.

Mahakama inatarajiwa kutoa mwongozo au uamuzi kuhusu uhalali wa notisi hiyo ya kuongeza ushahidi mpya katika hatua zijazo za kesi hiyo inayovuta hisia za wengi nchini.

The post Tundu Lissu Apinga Ushahidi Mpya Katika Kesi ya Uhaini appeared first on Global Publishers.



Prev Post Mufti Aomboleza Kifo cha Kardinali Pengo Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph – Video
Next Post Video: Ajali Kubwa Kwa Idd, Arumeru: Basi la Dar Express Lagongwa na Daladala
Related Posts
Comments 1
  • Brettaddet

    Informationbreach – Know If Your Data Is Already Leaked
    Massive data breaches happen every day. Check if your email, credit info, or personal data appears in leaked or hacked databases.
    Scan 33B+ leaked passwords and 50M new breach records daily to detect exposure instantly.
    Get breach alerts, see if your accounts are in credit card leaks, email breaches, or hacked dumps — all in one click.
    Protect yourself from identity theft for just $2 — your breach awareness shield starts now.
    Check Your Exposure Now: <a href=https://informationbreach.net> Cyber breach at target</a>

    |

    24 Feb 2026
Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook