Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Mirambo Ashinda Kwa Kishindo Uenyekiti CUF, Achukua Nafasi Ya Prof. Lipumba

  • 22
Scroll Down To Discover

Chama cha Wananchi (CUF) kimempata Mwenyekiti mpya wa Taifa, ambapo Mirambo Camil Yusuf amechaguliwa kushika nafasi hiyo akichukua mikoba ya Ibrahim Lipumba, aliyekuwa akiiongoza tangu mwaka 1999.

Matokeo hayo yametangazwa Februari 22, 2026 na Mwenyekiti wa Uchaguzi wa chama hicho, Said Miraji, baada ya mkutano mkuu wa dharura uliohudhuriwa na wajumbe 456.

Matokeo ya Uenyekiti Taifa

  • Mirambo Camil Yusuf – Kura 257

  • Othman Omar Dunga – Kura 177

  • Nkunyunyika Siwale – Kura 6

Jumla ya kura halali zilikuwa 448 huku kura 6 zikiharibika.

Mirambo, ambaye pia ni Mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Kigoma Mjini, sasa ataongoza chama hicho katika kipindi kipya cha uongozi.

Matokeo Mengine

Makamu Mwenyekiti Bara

  • Miraji Mtibwiliko – Kura 264

  • Mohammed Ngulangwa – Kura 88

  • Mussa Mbarouk – Kura 82

Makamu Mwenyekiti Zanzibar

  • Haroub Mohamed Shamsi – Kura 256

  • Mbarouk Seif Salim – Kura 171

  • Amina Rashid Salim – Alijitoa

Uchaguzi huo umeashiria mabadiliko makubwa ya uongozi ndani ya CUF baada ya takribani miongo miwili chini ya Profesa Lipumba.

The post Mirambo Ashinda Kwa Kishindo Uenyekiti CUF, Achukua Nafasi Ya Prof. Lipumba appeared first on Global Publishers.



Prev Post Hizi Ndio Browser za Kijanja Achana na Chrome na Firefox
Next Post Tume Ya Uchunguzi Yaongezewa Siku 42 Kukamilisha Ripoti
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook