Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

TAFADHARI KABLA YA DERBY, SIMBA WASISITIZA HAKI NA

  • 23
Scroll Down To Discover

MENEJA wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, ameweka wazi kuwa barua waliyoifikisha kwa Bodi ya Ligi Tanzania haikuwa na lengo la kugomea Kariakoo Derby, bali ni kuomba ufafanuzi juu ya baadhi ya maamuzi yaliyotolewa.

Hivi karibuni Simba waliiandikia bodi hiyo wakitaka maelezo ya kina kuhusu uamuzi wa kuhamisha uwanja wa mchezo huo, sambamba na kuhoji sababu za tangazo la mabadiliko hayo kutolewa na Ofisa Habari wa Yanga SC badala ya mamlaka husika zinazosimamia ligi.

Akizungumza kuhusu suala hilo, Ahmed alisisitiza kuwa dhamira ya barua yao ni kuhakikisha taratibu, kanuni na sheria zinafuatwa ipasavyo, bila kuleta taharuki kuelekea katika mchezo huo mkubwa unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wengi.

“Hatutaki taharuki kuelekea Derby. Tunachotaka ni kanuni, haki na sheria zifuatwe. Hatujasema popote kuwa tumegomea mechi, na tunaendelea na maandalizi yetu kuelekea michezo yetu ijayo,” amesema Ahmed.

Ameongeza kuwa kikosi chao kipo imara na kinaendelea na kampeni ya kusaka alama tatu katika kila mchezo uliopo mbele yao, wakilenga kuimarisha nafasi yao kwenye msimamo wa ligi.

Wakati mjadala huo ukiendelea, tayari kikosi cha Simba kimesafiri kuelekea Dodoma kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Tanzania Prisons utakaochezwa Jumapili hii katika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma, wakihitaji ushindi ili kujiweka katika nafasi nzuri zaidi kwenye mbio za ubingwa.

The post TAFADHARI KABLA YA DERBY, SIMBA WASISITIZA HAKI NA appeared first on Soka La Bongo.



Prev Post UKIJICHANGANYA KWA JKT TANZANIA UTAKULA NYINGI
Next Post KAMWE AWACHAMBUA WANAOCHANGANYA USHINDANI NA
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook