Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

UKIJICHANGANYA KWA JKT TANZANIA UTAKULA NYINGI

  • 23
Scroll Down To Discover

BAADA ya JKT Tanzania kushinda mabao 7-0 mbele ya wakongwe wa soka na mabingwa wa zamani wa Ligi Kuu Bara na ile ya Muungano miaka ya 1980, Pan Africans kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo ikiwa ni mechi ya Kombe la Shirikisho, wachezaji wa timu hiyo wamesema wakipata nafasi ya kufunga mabao mengi hawawezi kuichezea.

Wafungaji wa mabao hayo katika mechi hiyo ya hatua ya 64 Bora walikuwa ni Paul Peter alifunga mabao manne, Karim Mfaume bao moja na Edward Songo alifunga  mawili na kuing’oa Pan katika michuano hiyo kwa aibu kubwa.

Beki wa timu hiyo, Abdulrahim Seif Bausi amesemamatokeo ya mpira wa miguu hayana huruma, hivyo inapotokea fursa ya kufunga mabao mengi wanatakiwa kuyafunga kadri wawezavyo, bila kuona huruma wakitambua kuna wakati wa kicheko na maumivu.

“Tumekuwa na mwanzo mzuri kwa kushinda kwa kishindo, ilikuwa zamu ya Pan African kuumia, kwani matokeo ya soka ni ya kupokezana, kila mtu anatakiwa abebe mzigo wake mwenyewe na hiyo ni michuano ukipigwa unatoka,” amesemaBausi.

Kwa upande wa mshambuliaji wa timu hiyo, Songo aliyefunga mabao mawili katika mechi dakika za lala salama, alisema: “Ni heshima kwetu kufunga mabao mengi tumeandika rekodi, unaweza ukaona ni rahisi lakini kuna timu za Ligi Kuu ambazo zimeishatolewa katika michuano hiyo.”

Maoni ya kocha wa timu hiyo Ahmad Ally, amesema:”Tuna mechi za FA na za Ligi Kuu, ushindi huo unazidi kuchochea morali ya wachezaji kuwa juu, hakuna mechi rahisi inahitaji utayari na kujitoa.”

JKT imeungana na timu nyingine 31 kusubiri droo ya kucheza mechi za hatua ya 32 kusaka kwenda 16 Bora ikiwa ni mwanzo wa msako wa tiketi ya uwakilishi wa nchi katika michuano a CAF kwa msimu ujao. Bingwa wa michuano hiyo ushiriki Kombe la Shirikisho Afrika na msimu huu Azam FC na Singida Black Stars zilishiriki na kutolewa makundi ilizocheza kwa mara ya kwanza.

The post UKIJICHANGANYA KWA JKT TANZANIA UTAKULA NYINGI appeared first on Soka La Bongo.



Prev Post MGUNDA MENO NJE, AKIISIKILIZIA YANGA
Next Post TAFADHARI KABLA YA DERBY, SIMBA WASISITIZA HAKI NA
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook