Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Mfanyabiashara Atoeleka Kigoma Polisi Waanza Uchunguzi

  • 22
Scroll Down To Discover

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma limetangaza kuanza uchunguzi wa kina kufuatia taarifa za kutoweka kwa mfanyabiashara wa Soko la Buzebazeba, Mahamoud Juma Abdallah (25), anayedaiwa kuchukuliwa na watu wasiofahamika akiwa eneo lake la kazi.

Kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, ACP Philemon Makungu, Februari 20, 2026, tukio hilo liliripotiwa rasmi Februari 19 majira ya saa 09:00 asubuhi. Mahamoud, ambaye ni mkazi wa Mtaa wa Mwasenga katika Manispaa ya Kigoma Ujiji, anadaiwa kutoweka katika mazingira tatanishi akiwa kazini kwake sokoni.

“Uchunguzi utakapokamilika utabaini ukweli wa tuhuma hizo. Aidha, Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma linatoa wito kwa yeyote mwenye taarifa au ushahidi ambao utasaidia uchunguzi kukamilika kwa wakati aufikishe Polisi ili uweze kufanyiwa kazi kwa haraka”, imeeleza taarifa hiyo.

Wakati msako na uchunguzi ukiendelea, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma amewataka wakazi wa Kigoma Ujiji na mkoa mzima kwa ujumla kuwa watulivu. Polisi wameahidi kutoa mrejesho mara baada ya ukweli wa tukio hilo kubainika na hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wahusika wowote watakaobainika kuhusika na suala hilo.

The post Mfanyabiashara Atoeleka Kigoma Polisi Waanza Uchunguzi appeared first on Global Publishers.



Prev Post Dkt. Mwigulu Azindua Shule Mpya Ya Sekondari Ya Mbatakero
Next Post Adaiwa Kumnyonga James Kisa Kutoka Kimapenzi na EX Wake
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook