Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Video: Majambazi 9 Wakiri Kumuua Bodaboda Tabora, RC Chacha Aeleza

  • 29
Scroll Down To Discover

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha, ameeleza kuwa jumla ya watu tisa wanaodaiwa kuwa majambazi wamekamatwa kufuatia oparesheni maalum iliyofanyika mkoani humo baada ya tukio la mauaji ya dereva bodaboda.

Akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara, Chacha amesema watuhumiwa hao walikamatwa kupitia msako uliohusisha vyombo vya ulinzi na usalama, na kwamba baada ya mahojiano ya awali wamekiri kuhusika na tukio hilo.

Amesisitiza kuwa uongozi wa mkoa hautavumilia vitendo vya uhalifu vinavyohatarisha maisha ya wananchi, akibainisha kuwa yuko tayari kuchukua hatua kali zaidi kuhakikisha wahusika wote wanatiwa nguvuni.

Ameongeza kuwa oparesheni hiyo itaendelea hadi pale vyombo vya dola vitakapojiridhisha kuwa mtandao wote wa wahalifu umevunjwa, huku akitoa wito kwa wananchi kuendelea na shughuli zao za kila siku bila hofu yoyote.

 

The post Video: Majambazi 9 Wakiri Kumuua Bodaboda Tabora, RC Chacha Aeleza appeared first on Global Publishers.



Prev Post Alichokifanya Trump Huko Venezuela Siyo Kipya; Hizo ndo Tabia za Wababe Wa Dunia Hii!
Next Post SIMBA YATUMBUA SURA MPYA, WADHAMINI WASHIKILIA HISA
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook