Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

HESHIMA YA SIMBA IMETUKUTA TUKIWA HAI, AHMED

  • 24
Scroll Down To Discover

MENEJA wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba Sports Club, Ahmed Ally, ameibua mjadala mzito baada ya kueleza wazi kufurahishwa kwake na kuondolewa kwa timu zote za Tanzania katika michuano ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Ahmed amesisitiza kuwa furaha yake haitokani na kuitakia mabaya soka la Tanzania, bali ni kutokana na kurejea kwa heshima ya Simba ambayo kwa miaka ya hivi karibuni imekuwa ikipeperusha bendera ya nchi kimataifa, hasa kwa mafanikio ya kufuzu hatua ya robo fainali mara kwa mara.

Katika msimu huu wa mashindano ya CAF, Tanzania iliingiza jumla ya timu nne. Simba Sports Club na Young Africans Sports Club ziliiwakilisha nchi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, huku Azam Football Club na Singida Black Stars zikishiriki Kombe la Shirikisho Afrika. Hata hivyo, timu zote zimeishia hatua ya makundi na kushindwa kutinga robo fainali.

Kwa mujibu wa Ahmed, mafanikio ya Simba kufika robo fainali katika misimu iliyopita yalifanya baadhi ya watu kudharau hatua hiyo na kuiona kama jambo jepesi ambalo timu yoyote ingeweza kulifikia bila maandalizi makubwa.

Ameeleza kuwa safari ya kufika robo fainali si rahisi kama inavyoonekana, kwani huhitaji uwekezaji, mipango madhubuti, presha kubwa pamoja na mapambano mazito ndani na nje ya uwanja.

“Watu waliona kama robo fainali ni kitu cha kawaida tu. Wakaanza kubeza na kudhani kila timu inaweza kufika hapo kirahisi. Lakini ukweli ni kwamba kuna nguvu, juhudi na magumu mengi tuliyokuwa tunapitia hadi kufika hapo,” amesema Ahmed.

Ameongeza kuwa licha ya Simba kuumia kwa kushindwa kuvuka hatua ya makundi msimu huu, bado wanafarijika kuona kuwa hatua waliyokuwa wakifika na kubezwa sasa imeonekana si nyepesi kama ilivyodhaniwa, baada ya timu nyingine kushindwa kuvuka.

Ahmed pia amekumbusha kuwa Simba iliposhiriki hatua ya makundi kwa mara ya kwanza mwaka 2018, haikuishia hapo bali ilitinga robo fainali, jambo analodai linaonyesha uthabiti na ukubwa wa klabu hiyo katika anga la kimataifa.

“Heshima yetu imetukuta tukiwa hai,” amesema kwa msisitizo, akimaanisha kuwa mafanikio ya Simba sasa yanatambuliwa kwa vitendo baada ya wengine kushindwa kufikia viwango hivyo.

Kauli hiyo imeibua mjadala miongoni mwa mashabiki wa soka nchini, baadhi wakiiunga mkono kama kauli ya kujiamini na kujivunia mafanikio, huku wengine wakiona ni kejeli kwa wapinzani wao.

The post HESHIMA YA SIMBA IMETUKUTA TUKIWA HAI, AHMED appeared first on Soka La Bongo.



Prev Post SIMBA YAANZA SAFARI YA KUSAKA TIKETI CAF
Next Post SIMBA SAFARI YA UBINGWA MEJA JENERALI ISAMUHYO
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook