Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

NMB Yaitangaza Sekta ya Madini ya Tanzania Nchini Afrika Kusini

  • 28
Scroll Down To Discover


Waziri wa Madini wa Tanzania, Anthony Mavunde, akizungumza wakati wa Kongamano la Uwekezaji katika Mnyororo wa Thamani wa Madini Tanzania, lililoandaliwa na Breakthrough Attorneys kwa ushirikiano na Benki ya NMB

Benki ya NMB imewakilisha kikamilifu Tanzania katika maonesho ya uwekezaji ya Mining Indaba 2026, yaliyofanyika jijini Cape Town, Afrika Kusini, kuanzia Februari 8 hadi 11.

Kupitia maafisa wake waandamizi, waliongozwa na Bw. Nelson Karawa Mkuu wa Kitengo cha Biashara kwa makampuni pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Mauzo Idara ya Hazina, Bw. Jeremiah Lyimo, NMB ilitumia jukwaa hilo kuitangaza Tanzania na sekta yake ya madini miongoni mwa wawekezaji wa kimataifa, ikisisitiza nafasi ya nchi yetu kama mojawapo ya maeneo yenye fursa lukuki za uwekezaji na rasilimali nyingi za madini duniani


Waziri wa Madini wa Tanzania, Anthony Mavunde (4 kushoto), pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, James G. Bwana (5 kushoto), wakifuatilia kwa karibu shughuli za Kongamano la Uwekezaji katika Mnyororo wa Thamani wa Madini Tanzania lililofanyika Cape Town, Afrika Kusini.

Aidha, kama washiriki wengine kutoka Tanzania, NMB ilitumia fursa za mikutano na makongamano katika maonesho hayo kuonyesha ushiriki wake na mchango wake katika maendeleo ya sekta ya madini nchini, pamoja na utayari wake wa kushiriki katika kufadhili miradi ya kimkakati ya madini.

Kwa kushirikiana na kampuni za Breakthrough Attorneys na Invest Africa, NMB iliandaa Mkutano wa Waevekezaji wa ‘Investing in Tanzania Mineral Value Chain Conference’. Mkutano huo ulilenga kuwatambulisha wawekezaji wa kimataifa fursa nyingi za uwekezaji katika sekta ya madini hapa Tanzania na kuonesha kwamba mazingira ya biashara nchini tayari yameandaliwa kwa wawekezaji wa kimataifa.

Mkuu wa Kitengo cha Mauzo Idara ya Hazina kutoka Benki ya NMB, Jeremiah Lyimo, akichangia hoja wakati wa Kongamano la Uwekezaji katika Mnyororo wa Thamani wa Madini Tanzania lililofanyika Cape Town, Afrika Kusini.

Mkutano huo ulifunguliwa rasmi na Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde. Miongoni mwa waliohudhuria walikuwa Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Mhe.. James Bwana, pamoja na viongozi kutoka Wizara ya Madini, TISEZA, na Tume ya Madini.

Katika kongamano hilo, , Bw. Lyimo alitumia fursa hiyo kuonesha na kueleza kuwa Benki ya NMB ina uwezo mkubwa wa kifedha pamoja na uzoefu wa kusimamia mikataba mikubwa. Pia, alisisitiza nafasi muhimu ya benki katika kuwezesha upatikanaji wa fedha kutoka ndani na nje ya nchi kwa ajili ya miradi mikubwa katika sekta ya madini.


Wajumbe kutoka Benki ya NMB wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde (wa tatu kushoto) , pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Mhe. James G. Bwana (wa nne kushoto), wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Uwekezaji katika Mnyororo wa Thamani wa Madini Tanzania lililofanyika jijini Cape Town, Afrika Kusini.

The post NMB Yaitangaza Sekta ya Madini ya Tanzania Nchini Afrika Kusini appeared first on Global Publishers.



Prev Post RC Chalamila Azindua Kliniki ya Sheria Jijini Dar es Salaam
Next Post PITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO FEBRUARI 17, 2026
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook