Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Rais Samia Afanya Mazungumzo na Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed

  • 23
Scroll Down To Discover

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed pembezoni mwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Umoja wa Afrika, tarehe 14 Februari, 2026 jijini Addis Ababa, Ethiopia.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed, pembezoni mwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU), tarehe 14 Februari 2026, jijini Addis Ababa, Ethiopia.

Katika kikao hicho, viongozi hao wawili walijadili masuala ya kuimarisha ushirikiano wa pande mbili kati ya Tanzania na Ethiopia, hususan katika sekta za biashara, uwekezaji, miundombinu, nishati na usafiri wa anga.

Aidha, waligusia umuhimu wa mshikamano wa bara la Afrika katika kukabiliana na changamoto za kiuchumi na kijamii, sambamba na kuharakisha utekelezaji wa miradi ya kimkakati kupitia ajenda za Umoja wa Afrika.

Mazungumzo hayo yanaashiria dhamira ya mataifa hayo mawili kuendelea kukuza uhusiano wa kidiplomasia na kiuchumi kwa manufaa ya wananchi wake pamoja na maendeleo ya bara zima la Afrika.

The post Rais Samia Afanya Mazungumzo na Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed appeared first on Global Publishers.



Prev Post Rais Samia Akishiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Umoja wa Afrika 2026 – Video
Next Post Rich Mitindo Amzawadia Jackline Wolper Magari Mawili ya Kifahari Valentine
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook