Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

RC Chalamila Achukizwa na Kasi ndogo ya Utekelezaji wa Miradi ya BRT Kinondoni

  • 20
Scroll Down To Discover

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ameeleza kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wa barabara ya mwendokasi ya BRT phase 4  kuelekea tegeta baada ya kukuta ujenzi huo ukiwa chini ya asilimia 50 wakati unapaswa kuwa umefikia asilimia 65 ambapo ametoa muda wa wiki mbili za matazamio kwa wakandasasi wa mradi huo kuongeza kasi kabla hatua kuanza kuchukiliwa

Akizungumza wakatu anafanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya ujenzi wa daraja la mkwajuni na miradi ya ujenji wa barabara wilaya ya kinondoni Mkuu wa Mkoa Albert Chalamila pamoja na kuridhishwa na ujenzi wa daraja la mkwajuni amesema hayupo tayari kuoma Rais Dkt Samia akitoa fedha nyingi kwenye ujenzi wa barabara za mwendokasi ambazo hazikamiliki kwa wakati.

RC Chalamila amesisitiza kuwa baada ya wiki mbili atazitembelea tena barabara hizo na hatua za kisheria zitachukuliwa endapo hakutakuwa na ongezeko la kasi ya ujenzi huo, hivyo amewataka wakandarasi wanaojenga barabara hiyo kufamya kazi usiku na mchana ( Saa 24)

Akihitimisha ziara hiyo kwenye daraja la mtongani kata ya kunduchi Mkuu wa Mkoa Mhe Albert Chalamila ameeleza kuridhishwa na ujenzi wa daraja hilo na kufafanua namna ambavyo Rais Dkt Samia ametoa fedha kuboresha miundombinu ndani ya jiji hilo huki akotolea mifano ya daraja la nguva wilayani Kigamboni na mto mzinga wilayani Temeke ambako kote Rais Samia ametoa fedha

Aidha Meneja miradi msaidizi kutoka TANROAD Justin Moshi akatoa taarifa ya ujenzi wa mradi wa BRT 4 amesema mradi huo ulipaswa kuwa umekamilika hivyo uliongezwa muda lakini bado hatua nyingi hazijakamilika

Akiwa kwenye mradi wa ujenzi wadaraja la Mtongani ambalo lilibomoka kwa mvua Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Saad Mtambule ameeleza namna daraja hilo lilivyoleta usumbufu baada ya kubomoka

The post RC Chalamila Achukizwa na Kasi ndogo ya Utekelezaji wa Miradi ya BRT Kinondoni appeared first on Global Publishers.



Prev Post Rais Samia Ateua Wenyeviti wa Bodi Anne Makinda, Prof Maboko Na Wengine 3 -Video
Next Post Kamati ya Bunge Yaipongeza Tarura Kwa Kuimarisha Barabara, Kuokoa Maisha ya Wananchi
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook