Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Rais Samia Azindua Soko La Kisasa la Kariakoo (Picha +Video)

  • 27
Scroll Down To Discover

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 08 Februari, 2026, amezindua rasmi Soko la Kisasa la Kariakoo lililopo Jijini Dar es Salaam, hatua inayolenga kuimarisha biashara, usalama na mazingira bora ya kufanyia shughuli za kiuchumi kwa wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla.
Akikata utepe kuashiria uzinduzi wa soko hilo, Rais Samia amesema kuwa ujenzi wa soko la kisasa ni sehemu ya jitihada za Serikali katika kuboresha miundombinu ya biashara, kuongeza ajira na kukuza uchumi wa wananchi, hususan wafanyabiashara wadogo na wa kati.

Katika hotuba yake wakati wa uzinduzi huo, Rais Samia amewahimiza wafanyabiashara kulitumia soko hilo kwa kuzingatia usafi, nidhamu na ulipaji wa kodi, akisisitiza kuwa maendeleo ya taifa yanategemea ushirikiano kati ya Serikali na wananchi.

 


Soko la Kisasa la Kariakoo linatarajiwa kuwa kitovu muhimu cha biashara Jijini Dar es Salaam, likiwa na miundombinu ya kisasa ikiwemo maeneo ya biashara yaliyopangwa, huduma za usalama, usafi na miundombinu rafiki kwa wafanyabiashara na wateja.


Uzinduzi wa soko hilo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, wafanyabiashara pamoja na wananchi wa Jiji la Dar es Salaam.

 

The post Rais Samia Azindua Soko La Kisasa la Kariakoo (Picha +Video) appeared first on Global Publishers.



Prev Post Majambazi Watatu Wauawa Simiyu Wakifyatuliana Risasi na Polisi
Next Post Video: Gari Lililoibiwa Lakutwa Kwa Fundi Magari Songwe
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook