Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Majambazi 3 Wahukumiwa Kifungo Miaka 30, Unyang’anyi Kwa Kutumia Silaha

  • 33
Scroll Down To Discover

 


Mahakama ya Wilaya ya Kilindi imewahukumu Abdallah Ally Lusewa (31), Salehe Mohamed Lusewa (23) na Salehe Shaban Mngoya (43), wakazi wa Kijiji cha Songe Wilaya ya Kilindi, kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha.

Tukio hilo la unyang’anyi lilitokea Juni 18, 2025majira ya saa 22:47 usiku katika Kijiji cha Songe, ambapo mfanyabiashara Faraji Hamza Dole alivamiwa dukani kwake na kuibiwa mali mbalimbali zenye thamani ya shilingi 9,490,000/=.

Baada ya tukio kuripotiwa Polisi Songe – Kilindi, upelelezi ulianza mara moja na mnamo tarehe 17 Julai, 2025 mtuhumiwa Abdallah Ally Lusewa alikamatwa na kuwatia mbaroni wenzake. Katika upekuzi uliofanywa nyumbani kwa Salehe Shaban Mngoya, zilipatikana televisheni mbili zilizoibiwa.

Baada ya upelelezi kukamilika, watuhumiwa walifikishwa Mahakama ya Wilaya ya Kilindi chini ya kesi namba CC No. 19503/2025, na leo tarehe 06 Februari, 2026, Mahakama hiyo mbele ya Hakimu Bw. Toto Casmir iliwakuta na hatia na kuwahukumu kifungo cha miaka 30 jela.

The post Majambazi 3 Wahukumiwa Kifungo Miaka 30, Unyang’anyi Kwa Kutumia Silaha appeared first on Global Publishers.



Prev Post Museveni Amtunuku Nishani Mwanaye CDF Muhoozi Kwa Ujasiri
Next Post Zaidi ya Wananchi 3000 Wanufaika na Matibabu Bure Chalinze
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook