Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Wamiliki wa Mabasi NBS, Hood Wafariki, Sekta ya Mabasi Yapata Pigo – Video

  • 24
Scroll Down To Discover

Mfanyabiashara Nassor Hamdan Seif, maarufu kama Mzee NBS, mmiliki wa mabasi ya NBS Tabora, amefariki dunia jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Jijini Dar es Salaam. Mwili wa marehemu umehamishwa kuelekea Tabora ambapo familia na marafiki wanatarajiwa kushiriki katika mazishi yake.

Kwa upande mwingine, Mzee Hood, aliyekuwa mmiliki wa kampuni ya mabasi Hood Bus Limited, amefariki dunia leo akiwa Morogoro Mjini. Familia yake imesema kuwa taratibu za mazishi na ratiba rasmi zitatangazwa hivi karibuni. Msiba wake upo nyumbani kwa marehemu, karibu na Jamatini, Morogoro Mjini.

Vifo hivi vinaacha pengo kubwa katika sekta ya usafirishaji wa abiria nchini, huku wafuasi na wafanyakazi wa mabasi hao wakihisi huzuni kubwa kwa kuondokewa na viongozi hawa waliokuwa mashujaa wa biashara ya mabasi.

Familia na mashabiki wanatarajiwa kuendelea kutoa heshima zao kupitia ratiba itakayotangazwa hivi karibuni.

Mzee Hood, aliyekuwa mmiliki wa kampuni ya mabasi Hood Bus Limited

The post Wamiliki wa Mabasi NBS, Hood Wafariki, Sekta ya Mabasi Yapata Pigo – Video appeared first on Global Publishers.



Prev Post Marekani Yapunguza Ushuru kwa Bidhaa za India Baada ya Makubaliano Mapya
Next Post Simba Yatoa Tamko Baada ya Kukwama Kutinga Robo Fainali CAF
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook