Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Rais Samia Aanza Ziara ya Kikazi Dubai, Afanya Mazungumzo na Viongozi

  • 26
Scroll Down To Discover

Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jumanne, Februari 3 ameanza ziara ya kikazi Nchini Dubai, UAE kwa kufanya mazungumzo na viongozi na wadau wa kimataifa.

Katika ratiba ya leo, Rais Samia anakutana na Gaston Browne, Waziri Mkuu wa Antigua and Barbuda, pamoja na kufanya mazungumzo ya pande mbili na Bi. Shaikha Al Nuwais, Katibu Mkuu wa Shirika la Utalii la Umoja wa Mataifa (UN Tourism), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuimarisha ushirikiano, diplomasia ya kiuchumi na kuvutia uwekezaji wa moja kwa moja nchini.

Jioni ya leo, Rais Samia atashiriki uzinduzi wa Global Africa Investment Summit (GAIS)— jukwaa la uwekezaji linalolenga kuoanisha miradi iliyo tayari kuwekezeka barani Afrika na wawekezaji wa kimataifa.

GAIS ni mpango wa kimkakati unaoendeshwa sambamba na majadiliano ya sera ya World Governments Summit (WGS), kwa lengo la kubadili majadiliano ya sera kuwa uwekezaji halisi wenye matokeo.

The post Rais Samia Aanza Ziara ya Kikazi Dubai, Afanya Mazungumzo na Viongozi appeared first on Global Publishers.



Prev Post Waziri Mkuu Azindua Mpango wa Matrekta 10,000 Kuinua Sekta ya Kilimo
Next Post JK Kwa Mfalme Mswati Kujadili Upatikanaji Wa Fedha Za Miradi Ya Afya
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook