Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Morocco Yapokonywa Fursa ya Kuandaa Fainali ya Kombe la Dunia 2030

  • 29
Scroll Down To Discover

Morocco haitakuwa tena mwenyeji wa mechi ya fainali ya Kombe la Dunia la FIFA 2030, kufuatia matukio yaliyojitokeza wakati wa fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025, yaliyohusishwa na changamoto za usalama na usimamizi wa mashindano.

Kombe la Dunia la 2030 linatarajiwa kuandaliwa kwa pamoja na Uhispania, Ureno na Morocco, ambapo awali Morocco ilikuwa katika kinyang’anyiro cha kupewa heshima ya kuandaa mechi ya fainali ya michuano hiyo mikubwa duniani.

Hata hivyo, mizozo na matukio ya vurugu yaliyoripotiwa wakati wa fainali ya AFCON 2025 kati ya wenyeji Morocco na Senegal, yamezua wasiwasi mkubwa kuhusu uwezo wa nchi hiyo katika kudhibiti usalama na usimamizi wa matukio makubwa ya kimataifa.

Akithibitisha mabadiliko hayo, Rafael Louzán, Rais wa Shirikisho la Soka la Uhispania (RFEF), amesema kuwa Uhispania sasa imekabidhiwa rasmi jukumu la kuandaa mechi ya fainali ya Kombe la Dunia 2030, uamuzi uliofikiwa baada ya tathmini ya kina ya maandalizi na masuala ya kiusalama.

Uamuzi huo unaashiria pigo kwa ndoto ya Morocco kuandaa fainali ya Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza, huku Uhispania ikiongeza hadhi yake kama mmoja wa waandaaji wakuu wa mashindano hayo ya kihistoria.

The post Morocco Yapokonywa Fursa ya Kuandaa Fainali ya Kombe la Dunia 2030 appeared first on Global Publishers.



Prev Post Wabunge Wathibitisha Wenyeviti Wapya wa Bunge
Next Post NMB YAZINDUA MPANGO MKAKATI WA MUDA WA KATI WA MWAKA 2026 HADI 2030
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook