Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Mzee Edwin Mtei Aagwa Arusha, Serikali Kuenzi Mchango Wake Kitaifa

  • 52
Scroll Down To Discover

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika ibada ya kumuaga aliyekuwa Gavana wa kwanza wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Mzee Edwin Mtei, akimtaja kuwa kiongozi mahiri, mzalendo na nguzo muhimu katika historia ya uchumi na demokrasia ya Tanzania.

Akizungumza katika ibada hiyo ya mazishi iliyofanyika nyumbani kwa marehemu Tengeru, Dkt. Nchemba alisema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anatambua mchango mkubwa wa marehemu kwa Taifa na Serikali mara zote itaenzi mchango wake mkubwa katika uchumi na demokrasia nchini.

Waziri Mkuu alisema Mzee Mtei alikuwa miongoni mwa Watanzania wachache waliobahatika kuhudumu katika nyadhifa zote kuu za sekta ya fedha, ikiwemo kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Waziri wa Fedha na mwakilishi wa Tanzania katika taasisi za fedha za kimataifa, mchango uliompa heshima ya kipekee kitaifa na kimataifa.

Alisema katika maisha yake ya utumishi wa umma, marehemu alitambulika kwa kusimamia misingi ya uadilifu, uaminifu, uzalendo, bidii na kumcha Mungu na kwamba mchango wake uliweka msingi imara wa taasisi za kifedha na nidhamu ya uchumi wa Taifa.

Dkt. Nchemba alibainisha kuwa Mzee Mtei pia alikuwa miongoni mwa waasisi wa demokrasia ya vyama vingi nchini, akiwa mwanzilishi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), hatua iliyochangia kwa kiasi kikubwa kuimarisha mfumo wa kisiasa na uhuru wa mawazo nchini.

Katika kuenzi mchango wa marehemu kwa vitendo, Waziri Mkuu alitoa maelekezo mahsusi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo, akisisitiza kuwa hatua hizo ni sehemu ya kudumisha misingi ya maendeleo, haki na uzalendo aliyoyaishi marehemu.

The post Mzee Edwin Mtei Aagwa Arusha, Serikali Kuenzi Mchango Wake Kitaifa appeared first on Global Publishers.



Prev Post Gari la Maajabu: Fahamu 2026 Hyundai Palisade Calligraphy Hybrid AWD
Next Post ZAWADI USANASE ANAVYOIOKOA SIMBA QUEENS
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook