Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Waziri Mkuu Azindua Meli Mpya Mwanza ina Uwezo wa Kubeba Abiria 1,200

  • 54
Scroll Down To Discover

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, ameizindua rasmi meli ya kisasa ya MV New Mwanza, akisema ni uwekezaji wa kimkakati wa Serikali katika kuimarisha usafiri wa majini, kuongeza usalama wa abiria na kukuza uchumi wa Kanda ya Ziwa.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Dkt. Nchemba alisema Serikali imejidhatiti kuhakikisha usafiri wa majini unakuwa salama, wa uhakika na unaowanufaisha wananchi.

“Serikali imejidhatiti kuhakikisha usafiri wa majini unakuwa salama, wa uhakika na unaowanufaisha wananchi,” alisema Waziri Mkuu.

Meli ya MV New Mwanza ina uwezo wa kubeba abiria 1,200, mizigo hadi tani 400 na pia magari, ikijengwa kwa teknolojia ya kisasa ili kukidhi viwango vya usalama na huduma. Safari kati ya Mwanza na Bukoba itachukua takribani saa 6, ikitoa fursa ya usafiri wa haraka na wa uhakika kwa wasafiri na biashara.

Mradi huu umegharimu takribani USD 51.83 milioni, sawa na TSh bilioni 120.56, na unachukuliwa kuwa moja ya miradi muhimu ya maendeleo ya miundombinu ya usafiri wa majini nchini.

Uzinduzi wa MV New Mwanza unaonekana kuleta matumaini ya kuongeza ufanisi wa usafiri wa baharini katika Kanda ya Ziwa, hasa kwa kuwa meli hiyo itasaidia kupunguza mzigo wa barabara na kuongeza biashara kati ya mikoa ya ziwa.

MAREKANI YATUMA MELI za KIVITA KUELEKEA IRAN – TRUMPH ATHIBITISHA HUKU IRAN IKIJIPANGA 📍USA


 

The post Waziri Mkuu Azindua Meli Mpya Mwanza ina Uwezo wa Kubeba Abiria 1,200 appeared first on Global Publishers.



Prev Post Fahamu Gari la Maajabu linalomuwezesha Papa Kuwa Karibu na Waumini
Next Post PITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO JANUARI 24, 2026
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook