Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Serikali ya Uganda Yazima Intaneti Kuelekea Uchaguzi Mkuu

  • 42
Scroll Down To Discover

Mamlaka ya Mawasiliano ya Uganda imewaamuru watoa huduma za intaneti nchini humo kuzima huduma zao hadi itakapotangazwa tena.

Hatua hiyo inajiri wakati nchi hiyo ikielekea kwenye Uchaguzi wa Rais na Wabunge siku ya Alhamisi na inakuja baada ya kampeni kumalizika.

Katika barua iliyotolewa kwa Vyombo vya habari vya ndani, wakala wa Serikali iliwaandikia watoa huduma za mtandao, kuwataka kusubiri hadi taarifa zaidi kabla ya kurejesha huduma za mtandao.

Wiki iliyopita Mpinzani mkubwa wa Rais Yoweri Museveni, Robert Kyagulanyi Ssentamu, maarufu kama Bobi Wine alikuwa wa kwanza kutangaza kwamba Serikali ilipanga kuzima Mtandao wakati wa Uchaguzi, kama ilivyofanya wakati wa Uchaguzi wa 2021.

Wapinzani wanasema kwamba kuzimwa kwa mtandao kwa sasa ni jaribio la kufanya kazi mahali penye giza ambapo hakuna habari huru kuhusu maudhui yanayowafikia wananchi, isipokuwa yale yanayodhibitiwa na Serikali kupitia vyombo vyake vya habari.

The post Serikali ya Uganda Yazima Intaneti Kuelekea Uchaguzi Mkuu appeared first on Global Publishers.



Prev Post Man United Yakubaliana na Michael Carrick Kuwa Kocha Mkuu wa Muda
Next Post PSRS Yatangaza Nafasi 208 za Ajira Serikalini Taasisi 10 Mbalimbali
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook