Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Video: Marekani Yatingisha Iran, Trump Aonya Kabla ya Mazungumzo

  • 21
Scroll Down To Discover

Rais wa Marekani, Donald Trump amerudia maonyo yake ya kutaka kuingilia masuala ya Iran, akisema anaweza kuchukua hatua kabla ya kukutana na maafisa wa Iran kwa kuwa nchi hiyo imevuka mstari mwekundu.

Trump hajasema ni hatua gani anazokusudia kuchukua na alipoulizwa jana Jumatatu afafanue Iran imevuka mstari gani mwekundu, alisema:

“Ndiyo, inaonekana imevuka mstari mwekundu.Tunaangalia hili kwa umakini mkubwa. Jeshi pia linaangalia hili kwa umakini sana. Tunafikiria hatua kadhaa. Tutafanya uamuzi.”

Kundi la waangalizi lenye makao yake nchini Marekani, linasema zaidi ya watu 500 wamefariki dunia katika maandamano ya Iran tangu Desemba 28 mwaka jana.

RaisTrump tayari ameonya kwamba Marekani itaingilia kati kuwalinda waandamanaji nchini Iran ikiwa watazidi kuuawa.

Video imeibuka ya chumba cha kuhifadhia maiti cha muda kilichowekwa nje kidogo ya mji mkuu wa Iran, Tehran. Wairani wengi wamekwenda huko kuwatafuta wapendwa wao.

Kwa mujibu wa televisheni rasmi ya Iran, watu walionekana wakiwa wamebeba majeneza yenye miili ya askari wa vikosi vya usalama na raia katika majimbo 10 kwa ajili ya mazishi.

Wataalam na mashuhuda wanasema maandamano ya kupinga serikali nchini Iran yamekuwa makubwa kiasi kwamba hayajawahi kuonekana hapo awali katika historia ya miaka 47 tangu Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.

The post Video: Marekani Yatingisha Iran, Trump Aonya Kabla ya Mazungumzo appeared first on Global Publishers.



Prev Post Yajue Maajabu ya mwezi Februari, Waingia Kwenye Historia ya ‘Perfect Month 2026’
Next Post Kampeni za uchaguzi zapamba moto Uganda. Katika Dira ya Dunia TV
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook