Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Asia Mustapha Afariki Baada ya Kuishi Miaka 20 Bila Figo

  • 99
Scroll Down To Discover

Enzi za Uhai wake Asia Mustapha ni binti ambaye ameishi kwa takribani miaka 20 bila figo zote mbili akifanya mahojiano na Global TV

Habari mbaya zilizotufikia asubuhi hii ya Desemba 24, 2025 zinaeleza kuwa, mwanadada Asia Mustapha aliyesumbuliwa na figo kwa zaidi ya miaka 20 amefariki dunia.

Taarifa zilizothibitishwa na ndugu zake zinaeleza kuwa, Asia amekutwa na umauti usiku wa kuamkia leo alipokuwa amelazwa wodi ya wagonjwa mahututi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Asia alipitia mateso mazito tangu alipoanza kusumbuliwa na figo mwaka 2004 ambapo figo zake zilifeli zote hivyo ikabidi mwaka 2005 apandikizwe figo moja nchini India.

Baada ya kupandikizwa figo hiyo alikaa nayo hadi mwaka 2011 ambapo ilifeli tena na kuanzia hapo amekuwa akisafishwa damu kwa kutumia mashine (dialysis).

Kutokana na changamoto alizopitia katika maisha yake kuhusiana na figo, aliamua kuandika kitabu kinachoelezea maisha yake alichokipa jina la ‘NIMEISHI BILA FIGO MIAKA 20′.

Asia alisema kitabu hicho alikiandika kwa madhumuni ya kuwapa moyo wagonjwa wa figo na kuwaeleza kuwa kuumwa siyo mwisho wa maisha, kuwaelimisha wanaowauguza wagonjwa wa figo kuhusu chakula anachotakiwa kula mgonjwa, changamoto alizopitia na mengine mengi.

Kwa taarifa zaidi kuhusu msiba huo endelea kufuatilia GLOBAL TV…

Maziko yanatarajiwa kufanyika leo saa saba mchana katika Makaburi ya Kisutu, Jijini Dar es Salaam.

The post Asia Mustapha Afariki Baada ya Kuishi Miaka 20 Bila Figo appeared first on Global Publishers.



Prev Post Inspector Haroun atoa nyimbo mpya AI na Maisha Ndo Haya, Afunguka Mapaya – Video
Next Post Naibu Waziri aagiza tathmini ya kina kuhusu uendeshaji wa Kituo cha Mabasi Magufuli
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook