Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Awaonya Wanaopanga Vurugu

  • 64
Scroll Down To Discover

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, CPA Amos Makalla

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, CPA Amos Makalla, leo Jumatano Desemba 10, 2025, amewapongeza wananchi kwa kuyakataa maandamano ya Desemba 9, 2025, na amewataka kujenga utamaduni wa kudumu wa kukataa maandamano na matukio yote yenye viashiria vya uvunjifu wa amani mkoani Arusha.

Makalla amebainisha hayo wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za kibiashara katika Soko la Kilombero jijini Arusha, akiahidi kuwa serikali na vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Arusha vitaendelea kuhakikisha usalama na amani vinakuwepo.

Aidha, mbali na kuwahakikishia wananchi ulinzi na usalama muda wote, Makalla amehimiza umuhimu wa wananchi kujikita katika shughuli zao za kiuchumi na kijamii, akionya na kusisitiza utayari wa vyombo vya ulinzi na usalama kukabiliana na wote wanaopanga kufanya vitendo vya uhalifu na uvunjifu wa amani katika Mkoa wa Arusha.

POLISI WATOA ONYO ZITO WAASISI WA MAKUNDI YA UCHOCHEZI WATAFUTWA USIKU NA MCHANA

The post Mkuu wa Mkoa wa Arusha Awaonya Wanaopanga Vurugu appeared first on Global Publishers.



Prev Post Trump Aendeleza Mvutano na Ilhan Omar, Atupa Madai Mapya Yenye Utata
Next Post Kwa Nini Mercedes CLA 2026 Hybrid Imekuwa Gari Linalovutia Zaidi, Soma Hapa
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook