Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

TRA Yaibuka Kidedea Tuzo ya Uandaaji Hesabu Kwa Viwango vya Kimataifa

  • 72
Scroll Down To Discover

MAMLAKA ya Mapato tanzania (TRA), imeibuka Mshindi wa kwanza wa jumla katika tuzo ya Uandaaji wa Hesabu za Kifedha zinazozingatia viwango vya Kimataifa vya Uhasibu katika Sekta ya Umma (IPSAS), zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA). Pia imeibuka mshindi wa kwanza katika tuzo ya kipengele cha Taasisi za Serikali (Government Agency Categories).

Naibu Kamishina Mkuu wa TRA Mcha Hassan Mcha mara baada ya kupokea tuzo hiyo alisema, tuzo waliyopata ina umuhimu mkubwa, kwani inachangia kuonesha utendaji wao unakubalika Kimataifa.

Pia alisema tuzo hiyo inaonesha umahiri na ubunifu uliyopo kwa watumishi wa mamlaka hiyo.

”Tuzo hii ina umuhimu sana kwetu, inachangia kuonesha utendaji wetu unakubalika Kimataifa na ina waonesha Walipa Kodi kwamba kila shilingi inayokusanywa inafika katika mfuko Mkuu wa Serikali.”alisema

Vilevile Mcha aliwashukuru Walipa Kodi kwa kuendelea kulipa kwasababu TRA imeendelea kuvuka malengo ya ukusanyaji mapato kila mwaka.

Akizungumza jijini Dar es Salaam katika hafla ya kukabidhi tuzo hizo, Naibu Waziri wa Fedha Laurent Luswetula, alizipongeza taasisi zilizoibuka na ushindi, huku akisema wizara hiyo itaendelea kutoa ushirikiano kwa NBAA, ili kuendelea kuzalisha wahasibu na wakaguzi bora.

Pia alisema serikali itahakikisha NBAA inasimama imara ili iendelee kuzalisha watendaji bora kwa maslahi mapana ya taifa.

Vilevile Naibu Waziri huyo alipongeza NBAA kwa kuendelea kupanua wigo wa kuongeza washiriki kila mwaka.

Kwamujibu wa Mwenyekiti wa Bodi ya NBAA Profesa Slyivia Temu, katika hafla hiyo jumla ya taasisi 86 za Umma na binafsi zimeshiriki katika kujipima ubora wa kuwasilisha taarifa za fedha kwa mwaka 2024.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA Pius Maneno, lengo la tuzo hizo ni kuhakikisha taarifa za hesabu zinazotolewa zinakuwa na uwazi na uwajibikaji.

Alifafanua kuwa, tuzo hizo ni taarifa za hesabu za kuanzia Januari mwaka 2024 hadi Desemba, ambazo zimezalishwa kwa kufuata hesabu za Kimataifa na zilizopata hati safi.

The post TRA Yaibuka Kidedea Tuzo ya Uandaaji Hesabu Kwa Viwango vya Kimataifa appeared first on Global Publishers.



Prev Post Urusi Yapiga Hodi India Wakati Marekani Ikiongeza Ushuru wa Biashara
Next Post PITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO DISEMBA 06, 2025
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook