Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Urusi Yapiga Hodi India Wakati Marekani Ikiongeza Ushuru wa Biashara

  • 57
Scroll Down To Discover

Rais wa Urusi, Vladimir Putin, anaanza ziara ya siku mbili nchini India katika juhudi za kuimarisha ushirikiano, hususan katika sekta ya ulinzi. Ziara hii inafanyika wakati India inakabiliwa na shinikizo kubwa kutoka Marekani ikiitaka India iachane na ununuzi wa mafuta kutoka Urusi.

Ziara hiyo ni ya kwanza ya kiongozi huyo nchini humo tangu Urusi ilipoivamia Ukraine. Miongoni mwa ujumbe alioambatana nao Putin ni Waziri wa Ulinzi Andrei Belousov.

Rais huyo wa Urusi, anatarajiwa kukutana na Waziri Mkuu Narendra Modi watakaposhiriki pamoja dhifa maalumu ya faragha baadaye jioni.

Dhifa hiyo itafuatiwa na mkutano pamoja na mazungumzo na wafanya biashara yatakayofanyika Ijumaa.
Msemaji wa Ikulu ya Urusi, Kremlin, Dmitry Peskov, awali alieleza kuwa moja ya ajenda muhimu zitakazozungumziwa na viongozi hao wawili katika kuimarisha ushirikiano wa kiusalama ni pamoja na suala la Urusi kuipatia India mifumo ya ulinzi wa anga ya kisasa inayofahamika kama S-400.

Kando ya ushirikiano wa kiusalama, mahusiano ya kibiashara yanatarajiwa kuwemo kwenye ajenda ya mazungumzo mjini Delhi huku wizara ya mambo ya nje ikiuelezea ushirikiano kati ya nchi yake na Urusi kuwa ndiyo uhusiano thabiti zaidi katika nyakakati hizi.

Ziara ya Vladimir Putin inafanyika baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kuziwekea ushuru wa asilimia 50 bidhaa nyingi za India mnamo mwezi Agosti mwaka huu.

Hatua hiyo ilichukuliwa kama adhabu ya India kwa kununua mafuta ya Urusi.
India yenye idadi kubwa zaidi ya watu duniani imekuwa mnunuaji mkubwa wa mafuta hayo ya Urusi kwa bei nafuu na kuokoa mabilioni ya dola.

Hilo limeipa Moscow soko kubwa inalolihitaji baada ya wateja wake wakubwa wa Ulaya kusitisha kununua mafuta ya Urusi kwa sababu ya vita yake na Ukraine.

Duru za habari zinasema India inahofia kuwa makubaliano mapya ya nishati na usalama na Urusi yanaweza kumkasirisha Trump na matokeo yake yanaweza kuwa mabaya katika mazungumzo ya kibiashara yanayoendelea na Washington.

Hata hivyo msemaji wa Kremlin amebainisha kuwa Urusi kwa upande wake haijali lolote kuhusu ushuru wa Marekani.

The post Urusi Yapiga Hodi India Wakati Marekani Ikiongeza Ushuru wa Biashara appeared first on Global Publishers.



Prev Post Video: Polisi Yapiga Marufuku Maandamano ya Desemba 9, Yasifanyike Nchi Nzima
Next Post TRA Yaibuka Kidedea Tuzo ya Uandaaji Hesabu Kwa Viwango vya Kimataifa
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook