Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Video: Chalamila Aitaka TANESCO Kuchunguza Kauli ya Padri Kitima

  • 50
Scroll Down To Discover

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, ameielekeza TANESCO kuchukua hatua na kuchunguza kwa kina kauli iliyotolewa na Padri Dk. Charles Kitima akidai kuwa shirika hilo lilizima umeme ili kurahisisha shambulio dhidi yake katika makazi ya maaskofu.

Akizungumza leo katika hafla ya uzinduzi wa mita janja kwa wateja wa TANESCO jijini Dar es Salaam, Chalamila alisema madai hayo ni mazito na yanagusa moja kwa moja taswira ya shirika hilo muhimu la umma, hivyo hayawezi kupuuzwa.

Chalamila alieleza kuwa alimsikia Padri Kitima akitamka hadharani kuwa siku ya tukio la uvamizi kulikuwa na mpango kati ya wahalifu na TANESCO, kwa madai kwamba umeme umezimwa kwa makusudi ili kuwapa nafasi wavamizi kumdhuru.

Amesema tayari amezungumza na Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, Lazaro Twange, na wamekubaliana kuwa kauli kama hizo zinahitaji uthibitisho wa kina na hatua stahiki, ili kulinda heshima na uaminifu wa shirika hilo mbele ya wananchi.

Chalamila ameongeza kuwa kama kuna ukweli wowote, uchunguzi utafichua; na kama ni taarifa zisizo sahihi, hatua zitachukuliwa kwa mujibu wa taratibu.

The post Video: Chalamila Aitaka TANESCO Kuchunguza Kauli ya Padri Kitima appeared first on Global Publishers.



Prev Post Jeshi la polisi Tanzania lapiga marufuku maandamano ya Desemba 9. Katika Dira ya Dunia TV
Next Post Dkt. Mwigulu Akagua Uharibifu Kiwanda Cha Magodoro Cha Banco
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook