Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Polisi Tarime Rorya Wakanusha Taarifa za Kutekwa kwa Mkazi wa Gwitiryo

  • 77
Scroll Down To Discover

Jeshi la Polisi Mkoa wa Tarime Rorya limekanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni kuhusu kutekwa kwa Fredrick Mang’era Kemange maarufu British, mkazi wa Kijiji cha Gwitiryo Sirari likieleza kuwa linamshikilia kwa tuhuma za kuchapisha na kusambaza taarifa za uchochezi na kuhamasisha vurugu Desemba 09, 2025.

Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi imesema British amekamatwa Desemba 03, 2025 majira ya saa saba mchana akiwa hotelini na kufikishwa kituo cha polisi Sirari kwa hatua zaidi za kisheria.

Aidha, Jeshi la Polisi limesema litaendelea kuwasaka na kuwakamata wale wanaoendesha makundi mbalimbali, kuchapisha na kusambaza taarifa zenye maudhui ya kuhamasisha uhalifu katika mitandao ya kijamii.

The post Polisi Tarime Rorya Wakanusha Taarifa za Kutekwa kwa Mkazi wa Gwitiryo appeared first on Global Publishers.



Prev Post Polisi Morogoro Wafuatilia Kutoweka kwa Mtawa Silianus Korongo – Video
Next Post Top 10 ya Magari Yaliyonunuliwa Zaidi Tanzania Mwaka 2025
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook