Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Polisi Morogoro Wafuatilia Kutoweka kwa Mtawa Silianus Korongo – Video

  • 59
Scroll Down To Discover

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Alex Mkama.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro limesema linafuatilia taarifa za kutoweka kwa Mtawa aliyetambulika kwa jina la Silianus Korongo (49) Mkazi wa Mtaa na Kata ya Tungi, Manispaa ya Morogoro, ambaye ametoweka katika nyumba ya malezi ya Watawa wa Shirika la Ndugu Wadogo wa Franciscan (ORDER OF FRIARS MINOR -OFM ) tangu Disemba 1, 2025.

Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Alex Mkama, aliyoitoa Disemba 3, 2025 imeeleza kuwa Jeshi hilo lilipokea taarifa za kutoweka kwa Mtawa huyo, ikieleza kwamba mara ya mwisho alitoka kwa ajili ya kwenda kununua Vifaa vya Ujenzi na hakurejea

Kamanda Mkama amesema uchunguzi na ufuatiliaji unaendelea, huku Jeshi hilo likitoa wito kwa Mwananchi yeyote mwenye taarifa zinazoweza kusaidia kuhusu kutoweka kwa Mtawa huyo kuwasilisha taarifa hizo katika kituo chochote cha Polisi.

The post Polisi Morogoro Wafuatilia Kutoweka kwa Mtawa Silianus Korongo – Video appeared first on Global Publishers.



Prev Post Kesi ya Mange Kimambi Yaaahirishwa Hadi Januari 2026 – Sababu Ni Upelelezi Haujakamilika
Next Post Polisi Tarime Rorya Wakanusha Taarifa za Kutekwa kwa Mkazi wa Gwitiryo
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook