Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Waziri wa Ulinzi Nigeria Ajiuzulu, Jenerali Mstaafu Musa Ateuliwa Kuchukua Nafasi Yake

  • 67
Scroll Down To Discover

Waziri wa Ulinzi wa Nigeria, Mohammed Badaru Abubakar.

Waziri wa Ulinzi wa Nigeria, Mohammed Badaru Abubakar, amejiuzulu wadhifa wake kutokana na sababu za kiafya, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Rais Bola Ahmed Tinubu.

Kujiuzulu kwa Abubakar, mwenye umri wa miaka 63, kunakuja wakati ambapo Nigeria inapitia kipindi kigumu cha kiusalama, huku serikali ikikabiliwa na mashinikizo makubwa kutokana na ongezeko la matukio ya utekaji nyara katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Jenerali mstaafu Christopher Musa

Wiki iliyopita, Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa iliripoti kuwa watu 402 – wengi wao wakiwa wanafunzi wametekwa nyara tangu katikati ya mwezi Novemba.

Katika hatua ya kujaza nafasi hiyo, Rais Tinubu amemteua Jenerali mstaafu Christopher Musa, mwenye umri wa miaka 58. Jenerali Musa aliwahi kuhudumu kama Mkuu wa Majeshi ya Nigeria kuanzia Juni 2023 hadi Oktoba 2025 na amejulikana kwa utaalam wake katika mikakati ya kijeshi, hususan operesheni dhidi ya makundi ya kijihadi kaskazini-mashariki mwa nchi.

KESI KUPINGA TUME YA RAIS MAHAKAMA YATOA SIKU 7/ALIYEBAKWA NA DAKTARI AFUNGUKA-YEYE AFUKUZWA

The post Waziri wa Ulinzi Nigeria Ajiuzulu, Jenerali Mstaafu Musa Ateuliwa Kuchukua Nafasi Yake appeared first on Global Publishers.



Prev Post EWURA Yatangaza Bei Mpya za Mafuta Mwezi Disemba, 2025
Next Post Vodacom Tanzania yakabidhi Makapu ya Sikuu kwa wateja mkoani Mbeya
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook