Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

DART Yarejesha Huduma Za Mabasi Yaendao Haraka Awamu Ya Kwanza

  • 51
Scroll Down To Discover

WAKALA wa Mabasi yaendayo Haraka Dar es salaam (DART) imerejesha huduma za usafiri wa umma katika awamu ya kwanza, kuanzia Ubungo Terminal kuelekea Gerezani, Kivukoni na Muhimbili.

Huduma hiyo imerejea rasmi leo Novemba 28, 2025 katika maeneo tajwa ikiwa ni hatua ya mwanzo ya kurejea kwa huduma baada ya uharibifu mkubwa wa miundombinu uliofanyika Oktoba 29, mwaka huu.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma wa DART, William Gatambi ameeleza hayo akitoa ufafanuzi wa kuanza kurejea kwa huduma hizo baada ya tathmini iliyofanyika ili kubaini maeneo salama kwa ajili ya kurejesha huduma.

Gatambi amesema wamefanya hivyo wakati ukarabati katika vituo vilivyoathiriwa ukiendelea kwa awamu ili kuhakikisha mfumo mzima unarejea kikamilifu, huku akikiri kuwa kusitishwa kwa huduma kuliathiri sana wananchi, huku wengi wakilazimika kuhangaika kupata usafiri wa uhakika.

The post DART Yarejesha Huduma Za Mabasi Yaendao Haraka Awamu Ya Kwanza appeared first on Global Publishers.



Prev Post Tanzania Kuendeleza Ushirikiano wa Kidiplomasia na Jumuiya ya Kimataifa
Next Post Usiyoyajua Kuhusu Toyota Land Cruiser Gx-R, Gr-S Na Zx (Lc300 Series)
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook