Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Dkt. Nchimbi Aiwakilisha Tanzania Katika Uwekaji Jiwe la Msingi la Ukarabati wa TAZARA

  • 81
Scroll Down To Discover


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amewasili Jijini Lusaka nchini Zambia Novemba 19, 2025.

Makamu wa Rais anatarajiwa kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Uzinduzi wa Ukarabati Mkubwa wa Reli ya TAZARA itakayofanyika tarehe 20 Novemba 2025 Jijini Lusaka.

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kenneth Kaunda, Makamu wa Rais amepokelewa na Waziri wa Afya wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Dkt. Elijah Muchima, Balozi wa Tanzania nchini Zambia Mhe. Balozi, Luteni Jenerali Mathew Mkingule, Maafisa waandamizi wa Jamhuri ya Zambia na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na vikundi mbalimbali vya ngoma vilivyoandaliwa kwa heshima yake.

Pamoja na viongozi wengine, Makamu wa Rais Dkt. Nchimbi ameambatana na Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi Prof. Godius Kahyarara, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Mhandisi Machibya Masanja pamoja Mkurugenzi Mkuu TASAC Bw. Mohamed Salum.

CHADEMA WAGOMEA UTEUZI WA TUME/CCM YATOA ONYO KALI/MAWAZIRI KUTUMBULIWA..UCHAMBUZI WA KAMATI



Prev Post Rais Samia na Rais Museveni Watunukiwa Tuzo za Heshima na CAF
Next Post USIMAMIZI WA BoT WAZIBA MIANYA YA DHULUMA NA UTAPELI KWENYE VIKUNDI/VIKOBA
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook