Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

USIMAMIZI WA BoT WAZIBA MIANYA YA DHULUMA NA UTAPELI KWENYE VIKUNDI/VIKOBA

  • 31
Scroll Down To Discover

Na Mwamvua Mwinyi, Dodoma

Novemba 20, 2025

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesisitiza umuhimu wa kusajili vikundi vya kifedha, ikieleza kuwa hatua hiyo imechangia kwa kiwango kikubwa kupunguza vilio, malalamiko na migogoro ya kifedha iliyokuwa ikiwakabili wanachama wengi kwa miaka mingi. 

Kupitia usimamizi wa karibu unaofanywa chini ya Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018, BoT imesema kumekuwa na mabadiliko makubwa katika ulinzi wa fedha za wananchi na uwajibikaji wa viongozi wa vikundi.

Katika mafunzo ya waandishi wa habari za uchumi na biashara Novemba 20,2025 inayoendelea jijini Dodoma, BoT ilieleza ufuatiliaji wa mifumo ya huduma ndogo za fedha sasa umeleta matokeo halisi, ikiwemo kupungua kwa kesi za kuvunjiana vibubu, kutokulipa mikopo, utoaji wa mikopo kandamizi na kuwekwa rehani mali kubwa kama magari na nyumba kinyume cha utaratibu. 

Meneja wa Usimamizi wa Huduma Ndogo za Fedha wa BoT, Dickson Gama alieleza ,mojawapo ya chanzo cha vilio na migogoro ndani ya VICOBA ni kuendesha shughuli bila usajili na bila kuwa na mkaguzi. 

“Hali hii imekuwa ikisababisha viongozi kutumia fedha vibaya, kutotenda haki, au kuwabebesha wanachama masharti magumu yasiyoeleweka. “Vikundi vinavyoendesha VICOBA bila kusajiliwa vinafanya kosa kisheria”

“Adhabu yake ni faini ya milioni moja hadi milioni 10, kifungo cha miaka miwili hadi mitano au vyote kwa pamoja,” alisisitiza.

Akitoa tathmini ya utekelezaji, Gama alibainisha hadi kufikia Septemba mwaka huu jumla ya vikundi 70,800 vya kijamii vimeshasajiliwa nchini ,Saccos 987 kupitia Wezesha Portal, mfumo wa kidijitali unaoratibiwa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI. 

“Usajili si taratibu za kiwandishi tu, ni ngao ya kulinda fedha na usalama wa wanachama,” alieleza. 

Ofisa Sheria Mwandamizi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Ramadhan Myonga alikumbusha BoT pia jukumu lake la msingi ni kulinda amana za wananchi kwenye benki na kwa watoa huduma ndogo za fedha kupitia mfumo wa SEMA NA BoT, wananchi wanahimizwa kutoa taarifa kuhusu udanganyifu, malipo ya ziada, riba zisizoeleweka au kukosa taarifa sahihi za mikopo. 

Myonga aliifafanua malalamiko hayo, kwa mujibu wa BoT, huchakatwa haraka ili kuhakikisha hakuna mwananchi anayepoteza fedha kwa sababu ya kutokujua haki zake.

Aliwataka viongozi wa vikundi kuongeza uadilifu kwa kuboresha utunzaji wa kumbukumbu, kutumia mifumo ya kidijitali na kuhakikisha michango ya wanachama inasimamiwa kwa uwazi.



Prev Post Dkt. Nchimbi Aiwakilisha Tanzania Katika Uwekaji Jiwe la Msingi la Ukarabati wa TAZARA
Next Post Rais Ruto apigia debe utawala wake. Katika Dira ya Dunia TV
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook