
Ni maumivu yasiyoelezeka!
Mwanamama Zainabu, mkazi wa Mbezi Makabe jijini Dar, anapitia kipindi kigumu baada ya kukatwa ulimi mara sita kutokana na tatizo la saratani ya ulimi.
Kwa sasa, amebakizwa na robo tu ya ulimi, huku sehemu kubwa ikiwa imekatwa hali inayomfanya kushindwa kuongea wala kula kama kawaida.
Madaktari wamemshauri kusafiri kwenda nchini India kwa ajili ya mionzi maalum itakayosaidia kuzuia saratani hiyo isisambae hadi kwenye mishipa ya kichwa.
Safari hiyo inahitaji shilingi milioni 55, kiasi ambacho hana uwezo nacho kwa sasa.
Zainabu anahitaji msaada wako ili aweze kupona na kuendelea kuwalea watoto wake wadogo ambao bado wanamtegemea.
Kama moyo wako umeguswa, tafadhali mchangie kupitia:
0741 500073 — David Ibrahim












Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!